Katibu
wa Tume ya Maadili Zanzibar, Ndugu; Kubingwa Mashaka Simba akifunga mkutano
uliojadili nafasi ya vijana (kulia) Katibu wa Baraza la Vijana Taifa, Ndugu;
Khamis Faraji Abdalla (kushoto) Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana Taifa,
Ndugu; Mariam Ishau Abdalla.
Mwenyekiti
wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, Mhe: Assaa Ahmad Rashid akihutubia
mabaraza ya Vijana ya Wilaya za Magharibi na Mjini wakati alipofungua mkutano
uliojadili nafasi ya Vijana katika kukuza maadili uliofanyika katika ukumbi wa
Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni.
Afisa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Zanzibar, Ndugu; Haji Juma Chapa, akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na
Wajumbe wa Mabaraza ya Vijana Wilaya za Magharibi na Mjini katika mkutano uliojadili
nafasi ya vijana katika kukuza maadili ulioandaliwa na Tume ya Maadili kwa
Mabaraza hayo. Pembeni yake Ndugu; Khamis Faraji Abdalla, Katibu wa Baraza la
Vijana Taifa Zanzibar.
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana Taifa kutoka Wilaya Magharibi B, Ndugu;
Said Moh’d akichangia mada katika mkutano uliohusu nafasi ya vijana katika
kukuza maadili ulioandaliwa na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar kwa
Mabaraza ya Vijana za Wilaya za Mjini na Magharibi Unguja uliofanyika katika
ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni.
Baadhi ya wajumbe wa Mabaraza ya Vijana Wilaya za
Magharibi na Mjini wakifuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa na watendaji
wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika mkutano uliojadili nafasi ya
vijana katika kukuza maadili uliofanyika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil. wajumbe
wakifuatilia mada zinazowasilishwa na maofisa wa Tume ya Maadili
No comments:
Post a Comment