Habari za Punde

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini Akutana na Kamishna Jenerali wa Magereza.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, (Kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji



Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Phaustine Kasike mapema leo asubuhi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.

Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.

Vilevile Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.


“Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.