Habari za Punde

Mwenge wa Uhuru waendelea kutembezwa Wilaya ya Chakechake

 KIONGOZI wa mbio wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 Charles Frances Kabeho, akizindua kisanduku cha Rushwa katika jengo la ZSTC Madungu Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 KATIBU Tawala Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali, akisoma risala ya wananchi wa Chake Chake Pemba, katika maadhimisho ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika mkutano wa hadhara, mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa mkesha wa mwenge huko skuli ya Shamiani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akipokea mwenge wa uhuru wakati wa usomaji wa taarifa ya Wilaya ya Chake Chake, katika mkesha wa mwenge huko katika viwanja vya skuli ya Shamiani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Wilaya ya Mkoani Issa Juma Ali, akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbizaji wa mwenge Kitaifa, wakati wa Usomaji wa Taarifa ya Wilaya ya Chake Chake huko katika Viwanja vya skuli ya Shamiani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 AFISA mdhamini Wizara ya Vijana Sanaa Utamaduni na Michezo Pemba Fatma Hamad Rajab, akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbizaji wa mwenge Kitaifa, wakati wa mkesha wa mwenge huko katika skuli ya Shamiani Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid, akimkabidhi kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Charles Frances Kabeho Risala ya wananchi wa Chake Chake, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Mkesha wa Mwenge.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Frances Kabeho, akiwa na mkuu wa  Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid, wakipitia kwa makini ratiba ya Mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya skuli ya Shamiani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiwa ongozana na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Charles Frances Kabeho, wakiimba wimbo maalumu wa heshima, wakati wa mkesha wa mwenge katika uwanja wa Skuli ya Shamiani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)


WANAFUNZI wa Skuli ya Madungu, Shamiani na Michakaeni, wakisikiliza taarifa ya Wilaya ya Chake Chake katika mkesha wa mwenge wa uhuru huko katika vianja vya skuli ya Shamiani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.