Habari za Punde

TzIGF Yawataka Watumiaji wa Mtandao Kujua Haki na Wajibu.


 Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Dkt. Philip Filikunjombe, akizungumza wakati wa kufunga kongamano la kujadili matumizi ya mtandao na utawala lililofanyika Chuo cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
 Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
  Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Mratibu wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao (TzIGF), Rebecca Ryakitimbo, akizungumza katika kongamano hilo kuhusu matumizi ya mtandao.
 Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),  Jabhera Matoghoro, akizungumzia matumizi ya mtandao. Kushoto ni Mratibu wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao (TzIGF), Rebecca Ryakitimbo.
 Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo
 Mwakilishi kutoka Jamii Forums, Max Maxence, akizungumza.
 Mkuu wa Idara ya TEHAMA Chuo Kikuu cha Usafirisha (NIT), Edgar Telesphory, akizungumza.
 Mwakilishi kutoka Tanzania Youth Vission Association, Abdilah Lugome, akizungumza.
 Joy Wathagi kutoka nchini Kenya, akizungumza.
Mshiriki Peter Mmbando, akizungumza

Na Dotto Mwaibale

WATUMIAJI wa mitandao wametakiwa kujua haki na wajibu wanapotumia mtandao ili kuondoa mikanganyiko inayoweza kujitokeza kwa watumiaji dhidi ya serikali na makundi mengine.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mratibu wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao (TzIGF), Rebecca Ryakitimbo wakati wa kufunga kongamano la kujadili matumizi ya mtandao na utawala.

Alisema ni vizuri watumiaji wa mtandao wakajua haki na wajibu wakati wa matumizi ya mtandao.

Ryakitimo alisema hapa nchini limeundwa jukwaa la utawala wa mtandao litakaloshughulikia kutoa elimu juu ya masuala ya mtandao ikijumuisha masuala ya kisheria, wajibu wa mtumiaji wa mtandao pamoja na kutoa mapendekezo ya watumiaji wa serikalini katika kutengeneza sera zenye tija kwa mamlaka na watumiaji.

Alisema matumizi ya mtandao yamekuwa ni sehemu ya maisha ya binaadamu wa sasa ya kila siku ambapo watu wamekuwa wakitumia kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kujiajiri, kuwasiliana na hata kutoa na kupata elimu pia, kadri mawasiliano hayo ya mitandao yanavyozidi kukua, ndivyo mamlaka nazo zimeweza kuunda sera na sheria kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mitandao. 

Aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa nao uliunda jukwaa linaloshughulikia haki na wajibu wa watumiaji wa masuala ya mtandao, UNIGF. Hivyo hata nchi wananchama nao wameunda majukwaa kama hayo ili kuwa na kauli moja katika kutunga sera zinazokubalika kwa mamlaka na watumiaji ili kuleta usawa unaoleta uwajibikaji katika mitandao. 


Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Dkt. Philip Filikunjombe alisema kuwa jukwaa hilo limekuja wakati muafaka ambapo watumiaji wa mtandao wanaongezeka kwa kasi huku wengi bado hawajui sheria na kanuni zinataka nini kwa mtumiaji.

Baadhi ya watumiaji wa mtandao walisema kuwa ingawa jukwaa hilo lina mchanganyiko wa watu, hivyo wanantarajia uwakilishi mzuri serikalini siku za usoni, lakini jukwaa hilo limechelewa kwani serikali imekwishapitisha sheria walizozitaja kuwa ni kandamizi kwa watumiaji wa mitandao.

Jukwaa la utawala wa mtandao lipo pia kwa mataifa mengine ya Afrika ya Mashariki, Joy Wathagi kutoka nchini Kenya, anasema kuwa jukwaa hilo kwa nchini kwao linanguvu kubwa na linatoa maoni yanayozingatiwa katika uundwaji wa sera, huku serikali nayo ikitoa ushirikiano mkubwa kwa jukwaa: 


Jukwaa hilo liliandaa mjadala wa maoni na elimu, ambapo maoni mbalimbali ya wadau yalitolewa, fursa mbalimbali za kiuchumi na elimu kwa vijana kupitia mtandaoni yaliwekwa bayana.huku baadhi ya washiriki wakitoka mataifa mengine ya afrika ya mashariki ikiwemo kenya na wengine kutoka nchi zingine ikiwemo Afrika kusini na Nigeria walihudhuria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.