Habari za Punde

Mama Mwanamwema Shein Akitoa Mkono wa Eid Al Hajj Kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Mazizini na Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar.

NAIBU Waziri Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Shadya Mohammed akiwa na Mtoto Anisa Abdallah anayelelewa katika Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Fatma Gharib Bilal.
Mlezi Mkuu wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar Bi. Saida Ali Mohammed akitowa maelezo ya Watoto wanaoishi katika nyumba hiyo wakati wa hafla ya mkono wa Eid Al Hajj.
WATOTO wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Shadya Mohammed, akitowa salamo za Mkono wa Eid Al Hajj za Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika makaazi yao mazizini
NAIBU Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Shadya Mohammed akitowa Mkono wa Eid Al Hajj kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar,akimuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
 NAIBU Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Shadya Mohammed akitowa Mkono wa Eid Al Hajj kwa Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar akimuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein

NAIBU Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Shadya Mohammed akimsalimia Mtoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar Zahir Abdllah wakati wa hafla ya kutowa mkono wa Eid Al Hajj kwa Watoto hao katika makaazi yao mombasa Zanzibar .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.