Habari za Punde

Panya Alikula Sehemu ya Mguu Wangu Nikiwa Afrika Kusini - Mabbutt

Nilikuwa nimeenda kulala na usiku panya akaingia chumba changu cha kulala, akapanda kitandani na kuamua kula mguu wangu.

Aliyekuwa mlinzi wa England na Tottenham Gary Mabbutt anasema panya alikula sehemu ya mguu wake akilala alipokuwa kwenye likizo nchini Afrika Kusini.
Mabbut 57- alilazimika kurudi Uingereza kufanyiwa upasuaji na kukaa hopsitalini kwa muda wa wiki moja.
Mabbut ana ugonjwa wa kisukari na ahisi uchungu kwenyy mwili wake.
Kisa hicho kilitokea wiki sita zilizopita wakati akitembelea binti yake ambaye anafanya kazi kwenye mbuga ya wanyamapori ya Kruger.
"Nilikuwa nimeenda kulala na usiku panya akaingia chumba changu cha kulala, akapanda kitandani na kuamua kula mguu wangu,' alisema.
"Aliacha shimo kubwa kwenye mguu wangu hadi kwa mfupa, na akala chini ya mguu wangu.
Aliuma mguu wa binti yangu kwanza katika chumba kingine cha kulala, kisha akaja kwangu na kusema, Baba kitu kimeuma mguu wangu.
Baada ya saa moja hivi, Mabbutt akahisi kitu kikiuma kidole cha mguu wakati akilala, kisha akaona mguu wake umejaa damu.
Mabbut anasema bado anahitaji matibabu ya kila siku kwa majeraha yake.
Licha ya kuambiwa akiwa na miaka 17 aachane na kandanda, Mabbut alicheza mechi 611 kwenye taaluma yake ya miaka 16 huko Tottenham.
Anasema anajinduka dawa ya insulin mara saba kwa siku na kupima damu yake mara 10 kwa siku.
Mwaka 2016 nusura nipoteze mguu wake na nilifanyiwa upasuaji kutokana na kufunga kwa mishiba. Hawezi tena kukimbia wale kugonga mpira.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.