Habari za Punde

Timu ya JKU Yaibuka Kidedea Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora Uwanja wa Amaan Kwa Kuifunga Timu ya Opec Mabao 3-1.

Wachezaji wa Timu ya Opec wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya JKU kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora kuaza mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda mchezo huo kwa bao 3-1.
 Kikosi cha Timu ya Opec kutoka Kisiwani Pemba kinachoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza mchezo wao na Timu ya JKU mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

MSHAMBULIAJI wa Timu ya JKU Suweid Juma akimpita beki wa Timu ya Opec Suleiman Nassor, wakati wa michuano ya Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda bao 3-1MSHAMBULIAJI wa Timu ya Opec akimpita beki wa Timu ya JKU Is-Haka Othman, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda bao 3-1.
 BEKI wa Timu ya Opec Osward Emmanuel akimiliki mpira huku mchezaji wa timu ya JKU Suleiman Said akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya JKU imeshinda bao 3-1.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.