Habari za Punde

Vijana Zanzibar Wajitokea Kufanyiwa Majaribio ya Udereva Kwenda Kufanya Kazi Katika Nchi za Ughaibu.

Vijana mbalimbali wa maeneo ya Zanzibar wakiwa katika viwanja vya mpira vya maisara wakisubiri kufanyika udahilo wa udereva kwa ajili ya kupatiwa kazi katika nchi za Ughaibu zoezi hilo linafanya na Kampuni ya Almarai Compny Limited, ili kupata vijana wanaoweza kufanya kazi ya udereva katika Nchi za Ughaibuni.
Vijana wengi zanzibar wamehamasika na kujitokeza kwa wingi kutafuta nafasi hiyo ya kufanya kazi nje ya udereva nje ya Zanzibar ili kuweza kujiwezesha kiuchumi.
Vijana wakijaza fomu maalum kwa ajili ya kufanyia udahili huo wa udereva katika viwanja vya mpira maisara Zanzibar ili kupata fursa kuweza kuajiriwa katika Nchi za Ughaibuni.
Zoezi la usaili likiendelea kwa kuendesha gari katika usaili huo uliofanyika katika viwanja vya mpira maisara. likiendesha na mtaalam kutoka kampuni hiyo.   

Vijana wanaoomba nafasi ya kazi ya udereva katika Nchi za Ughaibu wakisubira zao yao kwenda kufanya majaribio hayo ya udereva katika viwanja hivyo vya maisara. zoezi hilo limefanyika leo asubuhi 26/8/2018. na kujitokeza vijana wengi kutafuta ajira hiyo. Vijana wanatakiwa kuazia umri wa miaka 24 mpaka 34. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.