Habari za Punde

DKT. KIJAJI: UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI

Na. WFM

Serikali imeeleza kuwa 
uwekezaji wa mishahara kwa 
wafanyakazi nchini ni 
jukumu la mfanyakazi 
mwenyewe kwa 
kuwa mshahara ni mali ya 
mfanyakazi hivyo anaweza 
kuutumia kwa kuwekeza au 
kuto kuwekeza.
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri 
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa 
akijibu maswali ya Mbunge wa Viti maalum Mhe. Mwantum 
Dau Haji, aliyetaka kujua Serikali inasema nini kuhusu 
uwekezaji wa mishahara kwa watumishi wa umma na 
kuwepo kwa ucheleweshaji wa mishahara kwa Watumishi wa 
Umma..

Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa upande wake inawalipa 
mishahara wafanyakazi wake kwa wakati kwa kuzingatia 
waraka wa Hazina namba 12 wa mwaka 2004 ambao 
unaitaka Serikali kulipa mishahara kabla ya tarehe 25 ya kila 
mwezi.

“Kumbukumbu za malipo ya mishahara kwa watumishi wa 
umma zinaonesha kuwa, kuanzia Julai 2017 hadi Agosti 
2018, watumishi walilipwa mishahara yao kati ya tarehe 20 
na 24 ya kila mwezi hivyo napenda kuliarifu Bunge lako 
Tukufu na umma kwa ujumla kuwa hakuna ucheleweshaji wa 
malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma” alieleza Dkt. 
Kijaji.

Aidha Serikali imekuwa ikiwatendea haki wafanyakazi wake 
katika upandishaji wa madaraja na kila mwaka wafanyakazi 
hupandishwa madaraja.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.