Habari za Punde

Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima Lafana Kisiwani Pemba.

MKUU wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali akiangalia moja ya lishe za watoto zinazotengenezwa na Mwalimu wa wanakisomo cha watu wazima Kutoka Ubago Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja Juliana Masanja, katikati ni Mkurugenzi wa Elimu Mbadala zanzibar Mashavu Ahmada Fakihi wakati wa maonyesho ya bidhaa za wanavizomo katika  juma la elimu ya watu wazima Kitaifa lililofanyika katika kituo cha elimu mbadala Wingwi Wilaya ya Micheweni
MKUU wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali, akizungumza na wanafunzi wa fani ya Uchongaji wa Fanicha, mara baada ya kukagua kazi zao za mikono wanaozitengeneza kufuatia kupata taaluma hiyo katika vyuo vya amali Kisiwani Pemba, wakati wa juma la elimu ya watu wazima Kitaifa lililofanyika katika kituo cha elimu mbadala Wingwi Wilaya ya Micheweni
 MKURUGENZI wa Idara ya Elimu Mbadala na Watu wazima Zanzibar, Mashavu Ahmada Fakihi, akizungumza na wazazi, wanafunzi, wanakisomo na wananchi katika kilele cha juma la elimu ya watu wazima huko katika kituo cha elimu mbadala Wingwi Wilaya ya Michewenii
MKUU wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali akizungumza na Walimu, wanakisomo, wazazi na wananchi wa Wingwi katika kilele cha juma la elimu la watu wazima kitaifa lililofanyika katika kituo cha elimu mbadala Wingwi Wilaya ya Micheweni
MKUU wa Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali, akimkabidhi zawadi mmoja ya walimu wanaosemesha elimu ya Watu wazima, Kisiwani Pemba wakati wa kilele cha juma la elimu ya watu wazima kitaifa, lililofanyika katika kituo cha elimu mbadala Wingwi Wilaya ya Micheweni
WAGENI mbali mbali waalikwa waliohudhuria katika kilele cha Juma la elimu ya watu wazima kitaifa, lililofanyika katika kituo cha elimu mbadala Wingwi Wilaya ya Micheweni
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.