Habari za Punde

Safari ya Zanzibar kuelekea katika mtazamo wa matarajio ya kuwa Dubai ya Afrika Mashariki inaanza kuchipua kidogo kidogo kufuatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutiliana saini Mkataba na Kampuni ya Kimataifa ya Mohammed Omar Bin Haider Holding Group { MOBH } ya Nchini Dubai.

Waziri wa Fedha Zanzibar Dr, Khalid Salum Mohamed Kulia na Mkurugenzi wa Bodi akiwa pia Meneja Mkuu wa  Kampuni hiyo Bwana Omar Mohammad Bin Haider  wakitia saini Mkataba wa Makubalino ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika masuala ya kuimarisha Uwekezaji kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Grand
Exelsior iliyopo katika M ji wa Al – Brsha Dubai. kutoka Kulia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akishuhudia tendo hilo la Kihistoria kwa Zanzibar katika
harakati za kunyanyua uchumi wake.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akibadilishani  Hati za mikataba baada ya kusaini na Mkurugenzi wa Bodi akiwa pia Meneja Mkuu wa  Kampuni hiyo Bwana Omar Mohammad Bin Haider,wana Omar Mohammad Bin Haider, kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika masuala ya kuimarisha Uwekezaji. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Kulia akimpongeza Meneja Mkuu wa  Kampuni hiyo. Bwana Omar Mohammad Bin Haider baada ya kukamilisha zoezi la kutia saini Waziri wa Fedha wa Zanzibar Dr. Khalid kati kati akishuhudia.

Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr., Khalid Salum Mohamed akitoa Hotuba katika chakula Maalum cha Mchana kilichoandaliwa na Kampuni Bwana Omar Mohammad Bin Haider mara baada ya kumalizika kwa hafla ya Utiaji saini.


Kampuni ya MOBH Holding Group Bwana Omar Mohammad Bin Haider mwenye  Kilemba Kati kati Kulia Yake Balozi Seif na Kushoto yake Dr. Khalid wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kampuni, Ubalozi Wa Tanzania Dubai na watendaji wa Kampuni hiyo mara baada ya kukamilkika kwa zoezi la utiaji saini.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.