Habari za Punde

Wahitimu wa Kidatu cha Sita 96 Zanzibar Wakabidhiwa Zawadi Walioahidiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Zilizotolewa na Mfadhi wa Kampuni ya Rom Solutions Ltd.

Komputa zilizotolewa na Kampuni ya Rom Solutions Ltd kwa ajili ya zawadi kwa Wanafunzi 96 waliofaulu kwa kiwango cha juu katika Mtihani wa Taifa wa Kidatu cha Sita Zanzibar, ahadi hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutowa zawadi hizo kwa Wanafunzi watakaofanya vizuri mitihani yao hiyo kwa mwaka wa masomo 2017/2018. hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar.
Mgeni rasmin Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza wakati wa hafla ya kuwazawadia Wahitimu wa Kidatu cha Sita Zanzibar kwa kufaulu kwa Division 1 na 2 katika Mitihani yao ya Taifa kwa mwaka wa masomo 2017/2018. Mkuu wa Mkoa Mhe. Ayoub Mohammed alitoa ahadi kuwazawadia Wanafunzi watakaofanya vizuri mitihani yao ya Kidatu cha Sita kwa Skuli 17 za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akiwatambvulisha Wadau wa kuendeleza Elimu alioshirikiana nao katika Kampeni yake ya Mimi na Wewe kwa kuinua kiwango cha Elimu Zanzibar,  
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akitowa nasaha zake na kuwahamasisha Wahitimu hao kuendelea kufanya vizuri masomo yao wanapojiunga Elimu ya Juu ili kufikia lengo lao la elimu. kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi zawadi yake Mhitimu wa Kidatu cha Sita kutoka Skuli ya Sekondari ya SOS Zanzibar Biubwa Khamis Ussi aliyepata Division   1.3,na katikatika Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi zawadi yake Mhitimu wa Kidatu cha Sita kutoka Skuli ya Sekondari ya lumumba Fahad Rashid Salum aliyepata Division 1.3, na katikatika Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi Wanafunzi wa Kidatu cha Sita Zanzibar 96, waliofanya vizuri masomo yao katika Mtihani wa Taifa, na kutowa nasaha zake na kuwataka kuendeleza ufahamu wao na kufanya vizuri masomo yao ya elimu ya Vyuo Vikuu. 
Baadhi ya Wahitimu wa Kidatu cha Sita mwaka 2017/2018 wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhiwa zawadi zao walioahidiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakifanya vizuri mitihani yao ya Taifa kwa mwaka wa masomo 2017/2018, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mnara wa Mapinduzi Square Michezani Zanzibar. 
Wasanii wa Bongo Salama Jabir na Cloud wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhiwa zawani Wahitimu wa Kidatu cha Sita wa Skuli za Sekondari 17 za Mkoa wa Mjini Magharini Unguja jumla ya Wanafunzi 96 waliofanya vizuri wamekabidhiwa Komputa mpakato. (Laptop)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.