Habari za Punde

Kutokuzingatiwa Kwa Usalama na Afya Sehemu za Kazi Kunaweza Kuleta Athari Kubwa za Kiuchumi Kwa Wafanyakazi.


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa kazi (OSHA) Paul Gyuna kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga wakati alipotembelea banda lao kunakoendelea kuna kofanyika maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano mjini hapa


 Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao
 Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao
  Mkaguzi wa Afya wa Osha Blandina Reubeni akimpima urefu mmoja wa wananchi waliotembelea banda lao
 Mkaguzi wa Afya (OSHA) Dkt Linda Katabari akimpima presha mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao leo
KUTOKUZINGATIWA kwa usalama na afya sehemu za kazi kunaweza kuleta athari kubwa ya kiuchumi kwa wafanyakazi kutokana na kwamba wanaweza kukumbana na majanga makubwa hali inayopelekea kuathiri shughuli zao na kila siku na kujirudisha nyuma kimaendeleo.
Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa kazi (OSHA) Paul Gyuna wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga kunakofanyika maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa.
Alisema wanatumia maonyesho hayo ya wiki ya vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo wamedhamiria kuwaeleza fursa wanazoweza kuzitumia ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Tunaangalia Usalama na Afya kwenye maeneo yao ya kazi…tunaelewa wameajiriwa lakini kuna changamoto nyingi wanazopita kutokana na kwamba wengi hawaelewi kuhusiana na mambo ya usalama na afya na kutokujua jinsi ya kujikinga na madhara hivyo tumekuja kutoa elimu”Alisema.
Alisema elimu wanayoitoa kwenye maonyesho hayo wanaamini wananchi wakishaijua wanaweza kujiepusha na athari za kazi hata ufanisi wa kazi utaongezeka na kuongeza kipato hatua itakayosaidia kuinua uchumi wao na jamii zinazowazunguka.
Hata hivyo alisema pia licha ya kutoa elimu hiyo lakini wanatumia wiki hiyo kufanya upimaji wa afya, presha uzito na urefu na kutoa ushauri ili kuweza kuwasaidia kuondokana na matatizo wanayokutwa nayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.