Habari za Punde

NAIBU WAZIRI MHE. JAPHET HASUNGA AONYA UKATAJI MITI OVYO MKOANI SONGWE

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza jana na wananchi kuhusu athari za ukataji miti ovyo  kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe. 
 Baadhi ya Watendaji aliokuwa ameongozana nao katika mkutano huo wa hadhara katika kijiji cha Isalalo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akimsikiliza huku akiwa anaandika swali analoulizwa na zungumza Ester Mwakanja kuhusiana  athari za ukataji miti ovyo  kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe. 
  1. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akisoma  karatasi  katika mkutano wa hadhara ulioufanya katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe
  2. ( PICNA NA LUSUNVU HELELA)

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amewaonya watu wenye tabia ya kukata miti ovyo kuwa Serikali hatosita kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na kushamiri kwa uharibifu wa misitu mkoani Songwe.

Ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe.

Amesema kufuatia kasi ya ukataji miti ovyo unaoendelea  kwa ajili ya mbao na nishati ya mkaa katika maeneo hayo kunatishia kutoweka kwa mvua wanayoitegemea kwa ajili kilimo cha mazao ya kahawa, mahindi pamoja na mazao mengine.

Amewaeleza Wananchi hao  kuwa uharibifu huo ukiendelea utaawathiri wao wenyewe  kwa vile   mvua itakoma kunyesha katika maeneo yao.

Amewataka wakikata mti wapande miti na wale wanaokata miti kwa ajili ya Nishati ya mkaa wafuate kanuni na sheria ili kuepuka kukabiliana na Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS)

Aidha, Mhe. Hasunga Amewataka Wananchi hao kuwa  hata pale inapotokea wanataka kukata mti wa mwembe uliopo katika nyumba zao wanatakiwa kuomba kibali kutoka TFS.

Pia,  Waziri Hasunga amewaagiza TFS itoe miche 10,000 kwa Kata ya Wasa msimu wa mvua utakapokaribia kufuatia ombi la mwanakijji Kasian Mwanjala alilowasilisha kwa Mhe. Hasunga kuwa wanataka kupanda miti ili wanakosa miche.

Katika hatua nyingine, Mhe.Hasunga ambaye ni Mbunge katika jimbo la Vwawa lililopo mkoani hapo amewahakikishia wananchi wake kuwa ifikapo mwakani kata ya Wasa itapata umeme wa REA hali itakayosaidia kuboresha maisha kwa wananchi wake.

"Moja ya ahadi yangu niliyoitoa kwenu ni kuhakikisha katika jimbo langu wananchi mnapata umeme, hadi sasa tayari nguzo za umeme zimeanza kuwekwa " amesema Mhe Hasunga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.