Habari za Punde

Halmashauri Wilaya ya Kaskazini B waagizwa kutafuta mbinu mbadala kumaliza udhalilishaji wilayani humo

Na Takdir Ali,                                                         14-11-2018.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Utawala bora na Idara maalum za Sms ya Baraza la Wawakilishi Machano Othman Said ameutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja kutafuta mbinu mbadala za kumaliza vitendo vya udhalilishaji vinavyaodaiwa kufanywa na Watu wasiojuilikana katika eneo la Fungurefu Wilaya ya Kaskazini “B”.
Ameseyasema hayo mara baada ya kusikiliza malalamiko ya Wafanyabiashara hao wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika eneo hilo.
Amefahamisha kuwa kitendo cha Wafanyabiashara hao kunyanganywa vitu vyao ikiwemo fedha Taslim hakileti Taswira nzuri jambo ambalo kama halikupatiwa ufumbuzi wa haraka linaweza kusababisha Maafa katika eneo hilo.
Mwenyekiti huyo ameitaka Halmashauri hiyo kushirikiana na Wananchi kwa kuanzisha mpango wa kuwakamata wahusika na kuwafikisha katika yombo vya sheria.
Nae Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja Omar Hassan amesema Kamati ya ulinzi na usalama itahakikisha inafatilia tukio hilo ili kuhakikisha inawatambua wahusika wa vitendo hivyo ambao vinahatarisha usalama wa Wananchi.
Mapemba Kiongozi wa Wafanyabiashara ya Madagaa katika eneo la Fungurefu  Shani Mgana Sharif amesema juzi majira ya saa nane za usiku walivamiwa na kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na Watu wasiojuilikana na kulazimishwa kutumia Dawa za za kulevya na hatimae kuingiliwa jambo ambalo limewaathiri kwa kiasi kikubwa.
Aidha Amesema lazima Serikali ilifuafuatilie kwa kina suala hilo ili waliondoshe tatizo hilo na Wananchi waendelee na Biashara zao bila usumbufu wowote.
Hata hivyo ameiomba Kamati hiyo kuishauri Serikali kurekebisha mapungufu yaliopo ikiwa na kutokuwepo kwa Ulinzi wa uhakikika na Mazingira ya kufanyia biashara kutoridhika.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.