Habari za Punde

Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Ndg. Shaka Hamdu, Asema Rais Magufuli ni Kiongozi Bora Barani Afrika.

KATIBU wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Open katika mahafali ya kwanza ya Shule hiyo.
KATIBU wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka akimkabidhi Cheti mwanafunzi wa Shule hiyo
Na Mwandishi Wetu, Morogoro.
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka  amesema Rais wa Jamguri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, amekuwa kiongozi bora katika Bara la Afrika na duniani kote kutokana na msimamo wake wa kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi kwa  maslahi ya umma.
Hayo ameyasema leo katika mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya Open iliyopo Mkoa wa Morogoro, amesema msimamo wa Dkt. Magufuli unapaswa kuigwa na viongozi wengine nchini ili kuzisimamia ipasavyo rasilimali za nchi zitumike kwa kuwanufaisha wananchi wote badala ya watu wachache.
Kupitia mahafali hayo Shaka amesema Juhudi zinazochukuliwa na serikali katika kuimarisha sekta ya elimu ni kubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, mchango wa sekta binafsi katika kudahili wanafunzi wa vyuo vya ufundi, mafunzo na elimu ya ufundi sambamba na kusimamia sera ya elimu na mafunzo ya ufundi kama ilivyoelekezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM.
Shaka amesema ili kufikia mafanikio endelevu ni lazima serikali iwe na muundo, mpangilio wa kisera, mfumo wa kioganaizesheni, uhamasishaji na mipango ya kukuza elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu na inabopidi hujiibadili kulingana na matakwa ya wakati.
Katibu huyo wa CCM, ameongeza kwamba mtu yryote anayedhani Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea imekufa yeye mwenyewe hajielewi kwani serikali  inaposomesha wanafunzi bure, kutafuta madawati, kulipa mishahara walimu, kujenga vyuo vikuu, kutafuta vifaa vya kufundishia, vitabu vya ziada na kiada, zahanati na hospitali ni utekelezaji chini ya siasa ya ujamaa.
Katika maelezo yake Shaka amasema Watanzania hawana shauku wala ndoto  ya kutaka mabadiliko ya utawala kwa kutegemea wenye mawazo duni  waliokosa dira na malengo huku serikali ya CCM ikijibadili, kimfumo na kisera kukidhi matakwa ya wakati katika sekta ya elimu.
Tofauti ya msingi ya viongozi CCM na wengine ni kuwa wanajikita katika  utundu unaoshikamaa na ubunifu wa masuala nyeti ya kisera na kimfumo  kwa muktadha wa kupima mwelekeo wa kiuchumi , diplomasia yenye manufaa  na mabadiliko ya kidunia kulingana na mahitaji ya wakati.
"Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Magufuli itabaki madarakani ikiamini siasa ya ujamaa tokea zama za sera za uchumi hodhi na hata baada ya ujio wa soko huria na utandawazi , haishikilii ukale ikiwa mbele yake kunahitajika mabadiliko ya msingi.
Leo hii kama utawauliza wananchi kumi watoe maoni kuhusu utawala wa serikali ya Rais Dk John Magufuli,wanane watamtaja ni kiongozi bora Afrika huku wawili kati yao watakosoa bila ya kuwa na nguvu ya hoja kwa kigezo hicho Serikali ya inayongozwa na Chama Cha Mapinduzi bado inaheshimika.", alisema Shaka.
Amesema Maisha ya watanzania kwa kiasi kikubwa ni ya kijamaa kwani kupendana kwao, kuheshimiana na kusaidiana kunatokana na kujengeka kwa fikra za ujamaa , umoja wa kitaifa bila kujali itikadi za kiasiasa ama ubaguzi wa aina yoyote mwingine.
Ameipongeza Serikali kupitia wizara ya elimu kwa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kisera ili kukidhi mahitaji ya nyakati kutengeneza wahitimu watakao kimbizana na mazingira ya kiuchumi na kisiasa kama ilivyoelekezwa katika ilani ya uchaguzi 2015/2020.
Aliwahimiza Watanzania kujenga matumaini na matarajio katika sera za chama cha Mapinduzi kwani ndicho chenye uwezo, ushahidi na uhodari wa kutenda jambo lolote ambalo haliwezi kufanywa na wengine nje ya mfumo  wa CCM.
Amewataka wanafunzi wasome kwa bidii na wale waliohitimu watambue wana jukumu la kujiandaa vyema kutumia fursa zinazotolewa na serikali kujiendeleza ili kulikabili soko la ajira chini.
CAPTION
Clip ya Shaka akihutubia katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya shule ya Sekondari ya Open Morogoro
Picha no.01-KATIBU wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka akiwahutubia wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Open katika mahafali ya kwanza ya Shule hiyo.
Picha no.KATIBU wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka akimkabidhi Cheti mwanafunzi wa Shule hiyo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.