Habari za Punde

SHERIA KUTUMIKA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI

 Mtaalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea,  Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Jacob Lusekelo akiwasilisha mada juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali  katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi , wakati wa mkutano wa wataalam wa afya moja Jijini Dar es salaam. 

Na. Mwandishi Maalum
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori, mifugo, mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo, wameanza mchakato wa kuandaa sheria ya kudhibiti athari za vimelea hatarishi kwa jamii, sheria hiyo itasimamia ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo.
Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua  kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi  pia wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea wakati  wa mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Usalama wa Afya na Ulinzi dhidi ya vimelea hatarishi vya magonjwa Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amebainisha kuwa serikali kupitia Dawati  la uratibu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu inategemea sana utaalamu wa kamati hiyo kutoa maoni yatakayojumuishwa katika sheria zitakazo simamia udhibiti wa vimelea hatarishi.  
 “Serikali itaendelea kuilinda jamii ya watanzania dhidi ya majanga yanayoweza kusababishwa na vimelea hatarishi ambavyo husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta majanga kwa jamii, kwa kulitambua hilo Ofisi ya Waziri Mkuu imeamua kuwakutanisha wataalamu husika ili watoe maoni yao juu ya udhibiti wenye nguvu ya kisheria” Amesema kanali Matamwe.
Nao waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph Masambu walibainisha kuwa udhibiti wa vimelea hatarishi ni muhimu kuwa na nguvu ya sheraia kwani kumekuwepo  na muingilianao mkubwa baina ya nchi mbalimbali,  ambapo muingiliano huo  hungeza milipuko ya magonjwa  kwa afya ya binadamu,     wanyama na mimea.
Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu, wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana Wizara ya Afya wameratibu mkutano huo kwa kupata wataalamu kutoka  Shirika la DTRA na Ufadhili wa CDC.
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (wa kwanza) akifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi Jijini Dares salaam.
 Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika majadiliano  wakati wa  mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika kutoa maoni ya  kuandaa sheria ya ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Dares salaam.
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika  picha ya pamoja mara baada ya  mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Dares salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.