Habari za Punde

Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania Bi Maniza Zaman Amtambulia Mkuu wa UNICEF Ofisi ya Zanzibar Bi.Maha Damjaj Kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Watoto {Unicef}Nchini Tanzania Bibi Maniza Zaman kwenye majengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani.



Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Watoto {Unicef}Nchini Tanzania Bibi Maniza Zaman akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na   Ujumbe wa Viongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto {Unicef} ulioongozwa na Mwakilishi wake Mkaazi Nchini Tanzania Bi. Maniza  Zaman.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akitambulishwa Mfanyakazi wa UNICEF Ofisi ya Zanzibar na Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania Bi,Maniza Zaman, baada ya mazungumzo yao yaliofanyika katika Ofisi yake Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akimzinkiliza Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania Bi. Maniza Zaman, alipofika katika Ofisi ya Balizi Seif katika jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani kumtambulisha Mkuu Mpya wa UNICEF Nchini Zanzibar.Bi. Maha Damaj.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akiagana na Mkuu Mpya wa UNICEF Ofisi ya Zanzibar Bi. Maha Damaj, baada ya hafla ya kutambulisha kwake iliofanyika katika Ofisi yake katika majengo ya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
(Picha na OMPR)
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa Mazungumzo na Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto {Unicef } Ofisini kwake ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Katika mazungumzo yao Mwakilishi Mkaazi wa Shirika hilo Nchini Tanzania Bibi Mariza Zaman aliyefika kumtambulisha Rasmi Mwakilishi wa Taasisi hiyo kwa upande wa Zanzibar Bibi Maha Damaj alisema Unicef itaendelea kuunga mkono miradi ya kijamii inayosimamiwa na Serikali Visiwani Zanzibar.
Bibi Marina Zaman alisema ushahidi wa hayo ni ule mradi wa pamoja kati ya SMZ na Unicef katika mikakati ya kukabiliana na maradhi mbali mbali yanayowasumbua Akina Mama na Watoto Wachanga.
Alisema zipo changamoto ambazo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalazimika kusaidiwa nguvu akizitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na mafunzo katika masuala ya kukabiliana na Maafa, mikakati ya kuendelea kudhibiti maradhi ya kuambukiza ambayo tayari yameshawahi kuleta maafa makubwa pamoja na taaluma ya kujiepusha na maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa Vijana na Wanawake.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru Uongozi wa Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa {Unicef} kupitia Wawakilishi wake hao kwa msaada mkubwa ulioipatia Zanzibar katika kujenga miundombinu kwenye Sekta ya Afya.
Balozi Seif  alisema Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika kampeni ya kudhibiti maradhi ya kuambukiza ya Kipindupindu jambo ambalo hakukuwa na kesi yoyote ya maradhi hayo iliyoripotiwa katika kituo chochote cha Afya mwaka uliopita.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimthibitishia Mwakilishi mpya wa Unicef atakayefanya kazi zake Zanzibar kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kumpa ushirikiano wakati wowote ili kufanikisha jukumu alilopangiwa na Taasisi hiyo ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.