Habari za Punde

Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund wa Abu Dhabi Watembelea Miradi ya Wajasiriamali Zanzibar.

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg.Juma Ali Juma, akizungumza na kutowa maelezo kuhusiana na  Mradi wa Wajasiriamali wa Tusizembee Cooperative wa Kisongoni Mfenesini wanaojishughulisha na ushagaji wa nafaka mbalimbali na mpunga wakati wa ziara ya Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund wa Abu Dhabi ulipotembelea Mradi huo, wakiwa  Zanzibar kwa ziara maalum.katikati Mkurugenzi wa Khalifa Fund Ndg. Nizar Cheniour, akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Bi. Maryam Juma Sadalla. 
Mkurugenzi wa Fakirice Milling Interprises Kisongoni Kinyasini Ndg.Yussuf Faki Yussuf, akitowamaelezo ya Ushirika wao kwa Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund, ulipotembelea Mradi wao huo wa mashine ya kusagia nafaka mbalimbali hasa mpunga husaka Tani Kumi kwa mwezi  na kusambasa katika mahoteli ya Kitalii Zanzibar na kwa Wananchi mbalimbali,kulia Mkurugenzi wa Mfuko wa Khalifa Fund Ndg. Nizar Cheniour na kulia Ofisa wa  Mkufo huo Ndg Ali Al Saadi, wakifuatilia maelezo hayo wakati walipotembelea Mradi huo Kinyasini Kisongoni Wilaya ya Kaskazini Unguja wakiwa katika ziara yao Zanzibar.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Khalifa Fund wa Abu Dhabi Ndg. Nizar Cheniour akizungumza wakati wa ziara yao kutembelea Mradi wa Ushirika wa Vijana wa Kisongoni wa Tusizembee Cooperative Kinyasini Kisongoni Wilaya ya Kaskazini Unguja Unguja wakati wa ziara yao. Zanzibar kutembelea Miradi ya Vijana.  
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Zanzibar Ndg. Juma Ali Juma, akizungumza na kutowa maelezo ya maendeleo ya Mradi wa Vijana wa Mashine ya kusagia nafaka na mpunga Kinyasini Kisongoni. 
Mashine ya Kisasa ya kusagia nafala ya Wajasiriamali wa Tusizembee Kinyasini Kisongoni.
Ujumbe wa Mfuko wa Khalifa Fund wakiwa katika Kikundi cha Wasasiriamali cha Tusizembee Kinyasini Kisingoni kinachojishughulisha na usagaji wa mpunga na nafaka mbalimbali wakiangalia mpunga unaosagwa  katika mashine ya Kikundi hicho wakati wa ziara yao kutembelea Vikundi vya Vijana Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.