Habari za Punde

Muungano wapata mashine ya maji kupitia mradi wa PAZA

Na.Mwandishi Wetu. 
Waakazi wa shehia ya Muungoni wilaya ya Kusini Unguja wamesema huduma ya maji safi na salama imepatika baada ya kupata mashine mpya ya kuvutia maji katika kisima kutokana na kuhamasika na Mradi wa kukuza uwajibikaji Zanzibar (PAZA) unaosimamiwa chama cha waandishi wahabari wanawake Zanzibar (TAMWA-ZANZIBAR).

Akizungumza na waandishi wa habari hizi Moja ya waakazi wa shehia hiyo bi Salama Ali Hamad (50) amesema mradi huo umesaidia kuwaletea visima vya maji safi na salama  ingiwa maji hayo yanachumvi kidogo lakini umeweza kuwaondolea tatizo sugu la maji.

Amesema Mradi wa PAZA umewawezesha wananchi wa Muungoni kuhamasika na kuweza kufuatilia njia za kutatua matatizo mengi ikiwemo tatizo la uchakavu jengo la afya ambapo limeboreshwa  na huduma zinapatikana ipasavyo.

Aidha amewashukuru watendaji kazi wa ofisi ya Halmashauri za wilaya kwa namna walivyowajibika katika kutekeleza majukumu yao kwa wakati na wananchi wameridhirika kwani tatizo la maji lilikua kubwa.

Amesema tatizo la ujenzi wa uzio wa katika skuli ya Muungoni halijatekelezwa wananchi wa muungoni wameshindwa kujua sababu ya kutojengwa ujenzi huo hivyo wameomba TAMWA kuendeleza Mradi wa PAZA ili matatizo yalioibuliwa yamalizike.

Kwa upande wa Asasi za kiraia na matandao wa ardhi wilaya ya kusini, Halda Nassor Haji ambae anawahamasisha waakazi wa shehia ya Kitogani na Muungoni amesema watendaji wa Halmashauri wameshafanya tathmini ya ujenzi wa uzio katika skuli hiyo lakini bado halijatiwa katika utaratibu  wa mpango wa matumizi ya kifedha(bajeti) hivyo amewaomba wananchi waendelee kustahamili watapewa taarifa ya ujenzi utakapokua tayari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.