Habari za Punde

Serikali Haitavumilia Wanaopotosha Wakulima

Na. Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewataka Wakulima kutokusikiliza maneno ya barabarani ya wapotoshaji na badala yake waendelee kuiamini Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Gavana Shilatu aliyasema hayo Leo Jumatano Januari 9, 2019 alipokutana na kufanya kikao na  Wakulima wakubwa wa Korosho wanaoishi Kata ya Mihambwe.

Gavana Shilatu amewataka Wakulima kusimama imara na kuwapuuza wale wote wanaopotosha maana halisia ya zoezi la uhakiki wa Korosho kwa Wakulima.

*"Rais Magufuli ameonyesha nia ya dhati ya kutaka kumkomboa kiuchumi Mkulima wa Korosho. Zoezi la uhakiki linafanywa kuhakikisha Mkulima halisia ananufaika na jasho lake na sote tupuuze maneno  ya vijiweni. Serikali ipo kwa ajili ya kusimamia haki na jasho la Mkulima linamnufaisha Mkulima mwenyewe. Serikali haitawavumilia wanaopotosha Wakulima, wanaopotosha nia njema ya Rais Magufuli Kwa Wakulima."* alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu alitoa ufafanuzi ikiwemo kujibu maswali ya Wakulima wa Korosho wa Mihambwe waliyokuwa nayo. 

*"Mambo Kama akaunti za Wakulima kutokufanya kazi, kuchanganya taarifa Kwa Mkulima ni baadhi tu ya changamoto ambazo kwenye zoezi la uhakiki zinarekebishwa. Nawasihi Wakulima kuwa wavumilivu."* alimalizia Gavana Shilatu.

Mpaka mwisho wa kikao Wakulima waliridhika na ufafanuzi na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha Kwa Serikali Kama desturi yao ilivyo.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi  ya Mtendaji kata ya Mihambwe kilihudhuliwa na Mtendaji Kata Mihambwe, Afisa Maendeleo kata ya Mihambwe, Serikali za Vijiji vilivyopo Mihambwe, Viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) wa Mihambwe pamoja na Wakulima wa Korosho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.