Habari za Punde

Wanawake 100 wafikiwa na Mradi wa PAZA



Jumla wa Wanawake 100 wa Shehia ya Muungano, Kitogani na Bwejuu wilaya ya kusini Unguja wamenufaika na elimu ya kukuza Uwajibikaji Zanzibar (PAZA) kupitia asasi za kiraia na mitandao ya ardhi ambapo elimu hiyo imewaletea maendeleo katika maakazi yao ikiwemo kuondokewa changamoto ya maji, afya na elimu.

Akizungumza na mwandishi wa habri hizi Mwana asasi za kiraia Halda Nassor Haji (32) amesema  amewahamasisha wanawake 100 elimu ya kukuza uwajibishaji katika shehia hizo ili waondokane matatizo katika maeneo hayo.

Amesema wana Asasi wote walipewa mafuzo na chama cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar (TAMWA-Zanzibar) kupitia Mradi wa Kukuza uwajibikaji Zanzibar (PAZA) na kuwataka elimu hiyo kuwafikishia wanawake wenzao vijijini.

Halda amesema wametumia njia ya mkutano kutoa elimu hiyo kwa akina mama ambapo pia kila mwanakijiji alipata fursa ya kuibua matatizo yalimkabili katika eneo lake.

Kwa upande wa wanufaika wa Mradi huo, Bi Wahida Khatib Ali (24) mkaazi wa Muungoni amesema kupitia mradi wa PAZA wanaelimika njia ya kuwafuata watendaji wa Halmashauri na kujua majukumu yao.

“Paza imenielimisha naweza kuandika barua ya malalamiko ya shida ya maji na kupeleka Halmashauri na kufuatilia hadi kufikia hatua ya mafanikio, tulihudhuria mkutano sisi wote tuwaweza kutatua matatizo yetu kwa sasa”  Amesema Wahida

Amesema ameridhika kwa kiwango cha juu, Mradi wa PAZA umewaondolea matatizo mengi, wilaya ya kusini ikiwemo tatizo la utoro kwa wanafunzi, shida ya mji safi na salama, ukarabati wa vitua vya afya na majengo ya Skuli.

Hajji Iddi Hassan (25) ni Mkaazi wa Kitogani akizungumzia Mradi huo naye ameomba watendaji wa Mradi wa PAZA kuendeleea na mradi kama hiyo kwa sababu bado watu wana muamko mdogo wa kuhudhuria mkutano ya kijiji kutokana na itikadi za kisiasa.

“Tunahitaji elimu zaidi katika kijiji chetu kwa kuelimishwa wananchi kwa sababu bado kuna baadhi yetu hawataki kushiriki katika vikao na mikutano wanapoitwa kutokana na itikadi zao za kisiasa” aliongeza.

Amesema baadhi ya watu wanapoitwa kuhudhuria kwenye kikao cha kijiji wanapuunza na kuendelea na shughuli zao na hatimae kukosa taarifa za maendeleo katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.