Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohemed Shein Amefanya Uteuzi leo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ.

i. Mkuu wa Wilaya ya Kati -Bibi Hamida Mussa Khamis.

ii. Naibu katibu Mkuu katika ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Bwana Khalid Abdalla Omar.

iii. Katibu Tawala wa Mkoa wa Kusini, Pemba - Bwana Abdulla Rashid Ali.

iv. Katibu Tawala Wilaya ya Chake Chake - Bwana Omar Juma Ali.

2. OFISI YA RAIS, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA.

i. Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti katika Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Bwana Yussuf Mohammed Ali.

ii. Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Bwana Bakari Khamis Muhidini.

3. WIZARA YA KATIBA NA SHERIA.

i. Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Katiba na Sheria- Bibi Daima Mohamed Mkalimoto.

ii. Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Katiba na Sheria - Bwana Juma Ali Simai.

4. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI.

i. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa  masuala ya Uvuvi na mazao ya baharini katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi- Dkt. Nariman Saleh Jidawi.

ii. Mkurugenzi wa Idara ya Uhakika wa Chakula na Lishe katika Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi- Bwana Hamadi Masoud Ali.

5. WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE.

i. Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) - Dr. Juma Mohammed Salum.

ii. Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji ya Zanzibar- Bwana Omar Said Ameir.

6. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA , MAJI NA NISHATI.

 Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati - Bwana  Yussuf Amour Ali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.