Habari za Punde

Mkutano wa Uzinduzi wa Club ya Wafanyabiasha Kisiwani Pemba NMB Business Club.

MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid (kushoto), akisalimiana na mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba, Abdalla Ali Said (Ngonda) baada ya kuchaguliwa kwake na wafanyabiashara wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara Pemba
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid, akizungumza na wafanyabiashara wa Pemba, wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Pemba, uzinduzi huo uliofanyika mjini chake chake
MWENYEKITI Mteuliwa wa klabu ya wafanyabiashara ya NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali Said (Ngonda), akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano wa uzinduzi wa klabu hiyo, mkutano uliofanyika mjini Chake Chake.
MENEJA wa NMB kanda ya Dar es Salam na Zanzibar, Badru Iddi akizungumzia malengo ya Benk ya NMB kanda yake kwa mwaka 2019, wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Pemba, hafla ya uzinduzi huo uliofanyika mjini Chake Chake 
MWAKILISHI kutoka NMB Loelia Kibasa, akiwasilisha mada kuhusu NMB na Idara ya biashara, wakati wa ufunguzi wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB kisiwani Pemba, halfa iliyofanyika mjini Chake Chake. 
 MTAALAMU wa Mfunzo ya Biashara kutoka EIB Erick Chrispin akiwasilisha mada ya mafunzo ya Biashara, wakati wa uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba, uzinduzi huo uliofanyika mjini chake chake

MWENYEKITI wa klabu ya Wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali Said, akimkabidhi cheti cha shukurani mmoja wa wafanyabiashara na mteja wa benk ya NMB Pemba, Mwanakhamis Khamis, wakati wa hafla ya uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara hafla iliyofanyika mjini Chake Chake. 

MWENYEKITI wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB Kisiwani Pemba Abdalla Ali Said, akimkabidhi cheti meneja wa NMB Tawi la Pemba Ahmed Nassor, kwa niaba ya mfanyabiashara Abdalla Nassor Abdalla, wakati wa hafla ya uzinduzi wa klabu ya wafanyabiashara hafla iliyofanyika mjini Chake Chake.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.