Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi Ziarani Kisiwani Pemba

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Mgogoni alipofika kukagua Mradi wa Kisima cha Maji safi na Salama katika Kijiji cha Kinyasini na Kwale.
Baadhi ya Wananchi wa Vijiji vya Kinyasini na Kwale ndani ya Jimbo la Mgogoni wakimsikiliza Balozi Seif alipofika kukagua Mradi wa Kisima cha Maji safi na Salama katika Kijiji cha Kinyasini na Kwale.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Mussa Ramadhan akitoa maelezo ya Mradi wa Kisima cha Maji safi na salama katika Kijiji cha Kinyasini Jimboni Mgogoni Mkoa Kaskazini Pemba.
 Nd. Mussa Ramadhan akifafanua jambo jinsi mradi huo utavyofaidisha Wananchi wa Vijiji vya Kinyasini na Kwale ndani ya Jimbo la Mgogoni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Kisima cha Maji safi na salama kilichochimbwa katika Kijiji cha Kinyasini Mgogoni kitakachokuwa na uwezo wa kutoa Lita 30,000 za Maji ndani ya Jimbo la Mgogoni.
Eneo lenye mtaro wa kusafirishia maji ya Mvua katika Kijiji cha Limbani Kifumbikai ambao umeleta athari pembezoni mwa Bara bara itokayo Wete kuelekea Chake Chake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea maelezo kutoka Wahandisi wa Idara ya Utunzaji na Ujenzi wa Bara bara {UUB} ya ujenzi wa Kuta Nne pembezoni mwa Bara bara ya Wete Chake Chake.
Muonekano wa Mtaro wa kupitishia Maji ya Mvua Mvua katika Kijiji cha Limbani Kifumbikai ambao umeleta athari pembezoni mwa Bara bara itokayo Wete kuelekea Chake Chake. Picha na – OMPR – ZNZ.

Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Miundombinu inayoendelea kutekelezwa na Serikali  katika kuimarisha huduma za Maji safi na salama Nchini imelenga kupunguza gharama kubwa za uagizaji  wa Dawa tofauti kutoka Nje ya Nchi kwa ajili ya tiba ya Wananchi.
Alisema maradhi mengi yanayowakumba Wananchi hasa katika kipindi cha msimu wa Mvua Kubwa huibuka kutokana na Wananchi kutumia Maji yasiyo salama kwa matumizi yao ya kila siku.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizunguma na Wananchi alipofika Kinyasini Jimbo la Mgogoni Mkoa wa Kaskazini Pemba kukagua Mradi wa Kisima cha Maji Safi na Salama unaotekelezwa na Serikali Kuu kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA}.
Alisema Chama cha Mapinduzi katika Ilani na Sera zake iliahidi kutoa huduma za maji safi na salama kwa Wananchi wake ambapo kwa sasa Ahadi hiyo zimekuwa zikitekelezwa na Serikali Zake zote mbili zilizopewa Mamlaka ya kuongoza Dola Nchini Tanzania.
“Naamini wazi kwamba Wananchi wakinywa maji safi na salama Serikali itapunguza gharama za ununuzi  wa Dawa ambazo zinaweza fedha hizo kutumika kwa masuala mengine ya Maendeleo”. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wananchi hao wa Jimbo la Mgogoni kwamba katika Uongozi wake anendelea kufuatilia Mradi huo hadi kukamilika kwake katika baadhi ya Vijiji vilivyobakia kupata huduma hiyo ya Maji safi na salama hivi sasa.
Aliwapongeza Wahandisi na Uongozi mzima wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} kwa jitihada kubwa wanayoendelea kuchukuwa ya usambazaji Huduma ya Maji safi kwa kujenga Miundombinu ya kudumu ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Alisema hiyo ni kazi nzito na ya muda mrefu ambayo Wananchi ambao hadi sasa bado hawajapata huduma hiyo wanalazimika kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi ambacho Serikali inajitahidi kutanzua changamiotoi hiyo muhimu katika ustawi wao wa kila Siku.
Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar {ZAWA} Nd.Mussa Ramadhan alisema Kisima hicho ambacho Mabomba yake tayari yameshaanza kusambazwa kwa umbali wa Kilomita Mbili Nukta Mbili kina uwezo wa kutoa Lita 30,000 kwa Siku.
Nd. Mussa alimueleza Balozi Seif  kwamba Rasilmali hiyo ya Maji safi kwa sasa yatawafaidisha Wananhi wa Vijiji vya Kinyasini na Kwale Ndani ya Jimbo la Mgogoni kazi iliyosita kwa muda kutokana na mvua kubwa za msimu huu wa masika.
Alisema Mradi huo pekee wa uchimbaji wa kisima cha Kinyasini Kwale pamoja na ulazaji wa Mabomba unatarajiwa kutumia Gharama ya Shilingi Milioni 206,250,000/- hadi kukamilikka kwake Fedha zinazotokana na Bajeti ya Serikali kupitia Wizara inayosimamia Maji.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa Mamlaka ya Maji Zanzibar alifafanua kwamba Tasisi hiyo inayosimamia huduma za Maji inaendeleza Mradi wa Uchimbaji wa Visima 21 Zanzibar ambapo kati ya hivyo Visima 15 vinachimbwa katika maeneo ya Kisiwa cha Unguja na Visima Sita katika Maeneo ya Pemba chini ya ufadhili wa Serikali ya Ras Al Khaimah.
Naye Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni Mheshimiwa Shehe Hamad Matar akitoa shukrani kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo lake alisema Jamii imekuwa ikushuhudia jinsi Chama cha Mapinduzi kupitia Serikali zake inavyotekeleza Ahadi iliyotoa wakati wa kuomba ridhaa ya kuongoza Dola ya Tanzania.
Mh. Matar alisema Serikali kupitia Taasisi zake inatekeleza ahadi hizo bila ya kugugumizi jambo ambalo limekuwa likileta faraja kwa Wananchi walio wengi hapa Nchini.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kukagua vikita vinavyojengwa pembezoni mwa Bara bara itokayo Wete kuelekea Chake Chake hapo katika Kijiji cha Limbani Kifumbikai.
Mhandisi Mkaazi wa Idara ya Utunzaji na Utengenezaji wa Bara bara Zanzibar {UUB} Kisiwani Pemba Mhandisi Khamis Masoud Khamis alisema Wahandisi wa Taasisi hiyo wamelazimika kuhami mazingira ya eneo hilo kufuatia mmong’onyoko mkubwa uliosababishwa na mvua kubwa za hivi karibuni.
Mhandisi Khamis alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba upo ukuta uliojengwa Mwezi Septemba Mwaka 2018 lakini mvua za Mwaka huu zimepelekea Wataalamu wake kujenga kuta nne ili kudhibiti hali ya kasi ya Maji ya mvua yanayotiririka katika msingi huo.
Alimuhakikishia Balozi Seif na Wananchi wote wanaopita eneo hilo kwamba kuta zinazoendelea kujengwa pembezonimwa Bara bara hiyo zinatarajiwa kuwa salama kutokana na umadhubuti wake unaozingatia Taaluma ya hali ya juu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.