Habari za Punde

Mkutano wa Wadau Kinachozungumzia Kuepeka na Madhara ya Dawa na Vifaa Tiba.

Wadau wa Dawa na Vifaa tiba wakijadili mwangozo uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuhakikisha matumizi ya dawa na vifaa tiba havileti madhara  kwa wananchi katika Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.

Picha na Makame Mshenga.

Na. Miza Kona   Maelezo Zanzibar.
Wakala Chakula na Dawa imeanza kujadili muongozo maalum uliotolewa na Jumuiya ya  Afrika Mashariki wenye lengo la kuinusuru jamii na athari zitakanazo na matumizi ya dawa ambayo hatimae husababisha madhara mbalimbali kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Afisa kutoka Wakala wa Dawa na Chakula Mohammed Omar kwenye Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe katika kikao cha wadau kinachojadili  hatua zinazofaa kuepukana na madhara ya dawa na vifaa tiba.
Amesema lengo la kikao hicho ni kutengeneza Muongozo ambao utawezesha kufuatilia madhara ya dawa, vifaatiba, tiba asili pamoja na chanjo ili kupata jamii yenye afya bora na kuepukana na maradhi yanayotokana na matumizi ya dawa.
Amesema muongozo huo pia utaweza kusaidia kuripoti, kuziwakilisha na kizitambua kuchunguza na kufuatilia dawa ambazo zinaleta madhara kwa jamii na kuzitafutia hatua za kuzipatia ufumbuzi kwa kutumia njia muafaka bila ya kubadilisha dhamira iliyowekwa na Jumuiya hiyo
Amefahamisha kuwa kumekuwa na matatizo makubwa ya madhara ya dawa ambazo husababisha kupata maradhi yasiyoambukiza kutokana na jamii kutotumia dawa bila ya kiwango kinachotakiwa.
“Dawa zina faida lakini pia madhara kadri unavyotumia dawa ndio madhara yanapoonekana hivyo tumeandaa muongozo wa kuweza kuzitambua dawa zenye kuleta madhara kwa jamii na kuzifanyia kazi kwa kuzifutia na kuzitambua ili kuweza kuisadia jamii”, alieleza Afisa huyo.  
Alisema wameweka fomu kila kituo cha Afya na hospitali kuzitambua dawa ambazo zinaleta madhara kwa jamii kwa kila mtumiaji ambae atapata madhara baada ya kutumia ili kupata ufumbuzi na kuisadia muongozo huo kufanyakazi yake lakini changamoto kubwa iliopo urejeshaji wa fomu hizo ni mdogo.
Nae MratibuMsaidizi wa Kitengo Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kikuu na Ukoma Issa Abeid Mussa amesema muongozo huo utaweza kujadi namna ya ufuatiliaji wa dawa na kuratibu athari zinazotokana na madhara utumiaji wa dawa       
Ameitaka Wakala wa Dawa na Chakula kuangalia kwa kina na kuzifuatilia dawa zote zinazoingizwa nchini kabla ya kuzisambaza katika vituo na kuzitumia ili kuepuka madhara kwa jamii.  
 CAPTION

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.