Habari za Punde

Ziara ya Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba

AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Pemba Ibrahim Saleh Juma, akitoa muhtaasari wa zaira ya kamati ya siasa Mkoa wa kaskazini kwa Wizara yake Pemba, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa bandari ya Wete. 
KAIMU Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Khadija Nassor Abdi,  akizungumza mara baada ya kupokea taarifa mbali mbali kutoka katika vituo vilivyopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipongo Pemba, wakati wa ziara ya kamati ya siasa mkoa huo kuangalia utekelezaji wa ilani ya CCM 2015/2020 kwa wizara hiyo
MDHAMINI wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Tawi la Pemba Habib Saleh Sultan, akitoa taarifa ya utekelezaji wa taasisi yake kwa miezi 10 kwa kamati ya siasa ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, ilipotembelea taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango Pemba
MENEJA wa Mapato na Matunzo Ali  Khatib Juma kutoka ZRB Pemba, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi kwa kipindi cha miezi 10 kwa kamati ya siasa ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, ilipotembelea vitengo vilivyochini ya Wizara ya Fedha na Mipango Pemba.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.