Habari za Punde

RC SHIGELLA AWATAKA MABAHARIA KUIMARISHA ULINZI ILI KUDHIBITI UINGIZWAJI WA DAWA ZA KULEVYAMKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani ambapo yanafanyika kwenye viwanja vya Lamore Jijini Tanga
MKURUGENZI wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katendo kwa niaba ya Katibu Katibu Mkuu.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la wakala wa meli Tanzania (TASAC) Emmanuel Ndomba akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Lamore Jijini Tanga
MKURUGENZI wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katendo kwa niaba ya Katibu Katibu Mkuu kushoto akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia wakati alipofika kwenye banda lao kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi.
MKURUGENZI wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Stella Katendo kwa niaba ya Katibu Katibu Mkuu kushoto akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia wakati alipofika kwenye banda lao kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi.
AFISA Mawasiliano wa Jeshi la Baharini (Nevy) mwenye cheo cha kawaida Ester Bundala kulia akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto Bendera wanazotumia kwenye mawasiliano.
AFISA Mawasiliano wa Jeshi la Baharini (Nevy) mwenye cheo cha kawaida Ester Bundala akionyesha bendera za mawasiliano wanazotumia
MENEJA Usajili ,Ukaguzi na Udhibiti wa Usalama wa Meli (TASAC) Mhandisi Alfred Waryana Misana kushoto akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia wakati alipotembelea mabanda kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akikagua boti
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Zena Saidi na Mkuu wa wilaya ya Tanga kulia Thobias Mwilapwa mara baada ya kufanya ufunguzi huo


MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewataka mabaharia kuhakikisha wanaimaimarisha ulinzi ili kuweza kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya ili watanzania wasiendelee kuathirika kwa namna moja ama nyengine na matumizi yake.

Shigella aliyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa Sherehe za Maadhimisho ya siku ya Mabaharia duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Lamore Jijini Tanga ambapo alisema mabaharia wanayodhamana kubwa baharini licha ya kukumbana na changamoto ikiwemo maharamia.

Licha ya hivyo lakini pia wanakumbana na watu wanaosafirtisha madawa ya kulevya bila kujua kuna mzigo umeigizwa hivyo lazima wahakikishe wanaimarisha ulinzi kila mara.

“Tukiimarisha shughuli za ulinzi madawa ya kulevya hayataweza kuingia na kuendelea kuathiri watanzania wasiendelee kuathiri kwa namna moja ama nyengine

Aidha Mkuu huyo wa mkoa alisema pia hali hiyo itasaidia kuzuia uingizwaji wa bidhaa ambazo zinaleta zikiwa hazikithi viwango na zinakuja kwa ajili ya kuathiri afya za watanzania hivyo tuna wajibu wa kulinda bidhaa tunazozisafirisha melini.

Mkuu huyo wa mkoa alisema pia kuhakikisha bidhaa inayokuja ni ile ambayo imefuata sheria za kuingia nchini ili serikali iweze kupata mapato yanayotokana na biashara zinazofanyika.

“La tatu tuna wajibu wa kulinda biashara ya binadamu isiendelee kwenye nchi yetu kwani hiyo inafanyika kwa kiasi kikubwa kwenye meli na mabaharia tuna wajibu wa kubaini kama watu wanaosafirishwa ni salama lakini pia wanazingatia sheria zilizopo kwenye nchi yetu”Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la wakala wa meli Tanzania (TASAC) Emmanuel Ndomba alisema kuwa wakati Sasa umefika wa kuwa na usawa wa kijinsia katika shughuli za ubaharia ili kuongeza fursa za ajira na kuinua uchumi wa nchi.

Alisema kuwa kutokana na kutekeleza sera ya viwanda kada hiyo ndio itakuwa na jukumu kubwa la kusafirisha shehena ya mizigo namalighafi hivyo ni muhimu kuwa na Raslimali watu ya kutosha.

"Hakuna uzalishaji unaoweza kufanyika bila ya kuhusisha sekta ya bahari hivyo ni vema serikali na wadau wengine kuona umuhimu wamabaharia ambao hufanikisha shughuli za usafiri katika bahari"alisema Ndomba.

Hata hivyo Kaimu Katibu Mkuu wa chama Cha mabahari Tanzania TASU Josiah Mwakibuja alisema kuwa wamiliki wa meli kutozingatia taratibu za mikataba na kusababisha kukosa haki zao wanazostahiki.

Pia aliiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa mabaharia ambao wanaojihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya ili waweze kujua madhara yake.

"Ukosefu wa ajira ya kudumu ni mmoja ya changamoto hivyo tunaiomba wizara ya uchukuzi pamoja namamlaka za TASAC na ZMA kuendelea kusimamia ipasavyo watumishi wa meli kwa kuchukuwa hatua stahiki kwa wamiliki wa meli endapo watabainika kutumia wafanyakazi wasio nasifa"alisema Mwakibuja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.