Habari za Punde

Timu ya Madaktari ya Madaktari wa Diaspora Kutoka Marekani wa Taasisi ya Head Inc. Wawasili Kisiwa Zanzibar Kutoa Huduma ya Afya Kwa Wananchi wa Pemba na Unguja.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Diaspora Zanzibar Bi.Adila Hilal Vuai, akiwapokea Madaktari wa Taasisi ya Head Inc Diaspora kutoka Nchini Marekani wakiwa katika bandari ya Malindi Zanzibar leo, tayari kwa kutoa huduma ya Afya kwa Wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba, Ujumbe huo wa Diaspora ukiondozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Head Inc Diaspora Bi. Asha Mustafa Nyanganyi kulia akiwa na baadhi ya Madaktari hao wakiwa katika bandari ya Zanzibar wakiwasili leo jioni.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Diaspora Zanzibar Ndugu Adila Hilal Vuai, akiwa na wageni wake Madaktari kutoka Taasisi ya Head Inc Diaspora ya Marekani walipowasili katika bandari ya Zanzibar leo, kwa ajili ya kuaza kambi ya kutowa huduma ya Afya kwa Wananchi wa Unguja na Pemba katika Hospital ya Chakechake Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.