Habari za Punde

ZFF laendelea na mchakato wa kuwaondoa wachezaji waliodanganya umri

Na Hawa Ally , 

SHIRIKISHO la Soka Zanzibar linaendelea na mchakato wake wa kuwatoa wachezaji ambao wamedanganya umri katika mikoa yake ya Zanzibar kuelekea Michuano ya TFF ya mikoa ya chini ya Umri wa 17 inayofanyika Tanzania Bara.

 Akizungumza na Waandishi wa habari Rais wa shirikisho hilo Seif Kombo alisema hatua hiyo Inafanyika baada ya kutokea udanganyifu wa Umri kwa wachezaji wane wa timu ya mkoa wa Mjini Magharibi ambao wameondoka jana kushiriki michuano hiyo.

 Alisema hatua hiyo ya imepelekeea timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi kusafiri na wachezaji 16 badala ya wachezaji 20 ambapo iwapo idadi hiyo ya wachezaji waliodanganya umri itaongezeka basi timu zitalazimika kurejea Zanzibar. 

 Alisema shirikisho hilo tayari limetuma wataalam kwenda Tanzania Bara kufanya uhakiki wa Umri kwa wachezaji wa mikoa yote ya Zanzibar na ripoti inatarajiwa kufika Leo usiku na kesho kufanyiwa kazi. Alisema kuwa ZFF haitamvumilia kiongozi yoyote aliyejihusisha na Sakata hilo la umri na badala yake itamchukulia hatua Ili liwe fundisho kwa wengine. 

"ZFF haitamuacha kiongozi ambae atajihusisha na unanganyifu wa umri hata kama atakuwa ni Kocha amehusika atachukuliwa hatua, ni aibu kwa Taifa timu kukutwa na udanganyifu wa Umri" 

Alisema katika udanganyifu wa Umri wanahusika wazazi, makocha na hata viongozi jambo ambalo linaweza kuwakosesha fursa wachezaji hao 

 Aidha akizungumzia juu ya michuano ya TFF ya mikoa ya chini ya Umri wa miaka 15 iliyomalizika mwezi huu alisema mchezaji bora aliyechaguliwa katika michuano hiyo kutoka katika timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi pia amekutwa na udanganyifu wa umri jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Soka la Zanzibar hususani kwa timu za Vijana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.