Habari za Punde

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dkt.Charles E Msonde Atangaza Matokeo ya Mitihani ya Kitadu cha Sita (ACSEE) Uliofanyika Mei 2019. Jumla ya Watahiuniwa 91,298 Walisajiliwa Kufanya Mtihani wa Kidatu Cha Sita.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dkt. Charles E.Msonde akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali Zanzibar wakati akitowa matokeo ya Mtihani wa Kidatu cha Sita (ACSEE) uliofanyika mwezi wa Mei 2019.
Amesema Jumla ya Watahiniwa 91,298 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidatu cha Sita 2019, wakiwemo Wasichana 37,948 (41.56%) na Wavulana 53,350 (58.44%) Kati ya watahiniwa waliosajiliwa wa Shule walikuwa 80,216 na wa Kujitegemea 11,082.  
Jumla ya Watahiniwa 88,069 sawa na asilimia 98.32, waliofanya mitihani ya kidatu cha sita mei 2019, wamefauulu vizuru kati ya Watahiniwa hao Wasichana waliofaulu ni 37,219 sawa na asilimia 99.11 na Wavulana waliofaulu ni 50,850 sawa na asilimia 97.75, amesema mwaka wa 2018 watahiniwa waliofaulu walikuwa 83,581 sawa na asilimia 97.58.
Amesema kwa Watahiniwa wa Shule kati ya watahiniwa 80,216, waliosajiliwa watahiniwa 79,770 sawa na asilimia 99.44 walifanya mtihani kati ya hao Wasichana walikuwa 33,883 (99.57%) na Wavulana 45.887 (99.35%) na Watahiniwa 446 (0.56%) hawakufanya mitihani.  
Katibu Mtendaji wa





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.