Habari za Punde

Kilimani City Yapata Viongozi Wapya

Na Hawa Ally.
Wanachama wa Klub ya kilimanicity kwa Mara nyingine wamemchagua Khamis Shalia chum  kuwa rais wa klub hiyo kwa kupata Kura 36 kati ya Kura 48 za wapiga  Kura wote waloshiriki uchaguzi huo uliofanyika hapo jana katika ukumbi wa chuo cha habari kilimani.

Akitamtangaza mshindi mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya klub hiyo Abduratif Ali alisema nafasi hiyo ilikuwa na  wagombea wawili ambapo mgombea Khamis Darueshi alipata Kura 11.

Kwa Upande wa Makamo wa rais Daud Mohmed aliibuka kidedea kwa kupata Kura 36, akimbwaga Kassim Chau aliyepata kura 12, Kwa upande wa Katibu wa klub hiyo Abrahamani Salum alishinda kwa kupata Kura Zote 48 huku makamo wake Azizi Iddi ambae alipata Kura 43 kati ya Kura 48 huku Kura Tano ziliharibika

Aidha kwa Upande wa Makamo mshika fedha Fadhir Omar alipata Kura 46 katika ya Kura Zote 48 huku Kura 2 ziliharibika, kwa Upande wa mshika fedha mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi alimtangaza Tawakar kombe ameshinda kwa kupata Kura 41 kati ya Kura Zote 48 huku Kura 7 ziliharibika. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.