Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Azungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara Kutoka Jimbo la Shadong Nchini China.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akifanya mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa Wafanyabiashara kutoka Jimbo la Shadong Nchini china Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Baadhi ya Viongozi wa Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Manispa ya Jimbo la Shadong ukimsikiliza Balozi Seif katika mazungumzo yao yaliyojikitazaidi katika masuala ya Uwekezaji.
Meya wa Manispa ya Jimbo la Shadong Bwana Zhaogang Wang akimueleza Balozi Seif azma ya Wawekezaji wa Jimbo lake kutaka kutumia fursa za Uwekezaji zilizopo Visiwani Zanzibar.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Viongozi wa Wafanyabiashara kutoka Manispa ya Jimbo la Shadong mara baada ya mazungumzo yao.
Picha na – OMPR – ZNZ.




Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa Wafanyabiashara kutoka Jimbo la Shadong Nchini china ukiongozwa na Meya wa Manispaa ya Mji wa Jimbo hilo Bwana Zhaogang Wang.
Katika mazungumzo yao Balozi Seif alisema Zanzibar bado ina fursa nyingi za Uwekezaji akatolea mfano Sekta Viwanda, Utalii, Mawasiliano na Biashara lakini mtazao wa sasa ni kuona eneo la Uvuvi wa Bahari Kuu linapewa Msukumo kama ilivyopewa Sekta ya Utalii.
Alisema Zanzibar imezunguukwa na Bahari sehemu zote mazingira ambayo Wawekezaji wa Jimbo la Shadong wanaweza kuitumia fursa hiyo kwa masuala ya uwekezaji kwa vile Nchi hiyo tayari imeshapiga hatua kubwa katika kuimarisha Uvuvi wa Bahari Kuu.
Balozi Seif alimuahidi Meya huyo wa Manispaa ya Shadong kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar muda wote itakuwa tayari kuwaunga mkon Wawekezaji wa Jimbo hilo na China kwa Ujumla pale watakapoamua kuanzisha miradi yao ya Kiuchumi Visiwani Zanzibar.
Mapema Meya wa Manispa ya Jimbo la Shadong Bwana Zhaogang Wang alisema China imefanya mabadiliko katika Sekta zake za Uwekezaji kwa kuwaruhusu Wafanyabiara Binafsi kuzitumia fursa hizo katika Mataifa mbali mbali Duniani.
Bwana Wang alisema ipo miradi ambayo Wawekezaji wa Jimbo hilo wameshaipanga katika mfumo wa Ubia na Taasisi tofauti Duniani zikiwemo Nchi za Bara la Afrika katika sekta za Uvuvi wa Bahari kuu pamoja na Kilimo cha kisasa.
Kwa upande wake Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshatliana saini Mkataba wa Ushirikiano kati yake na Uongozi wa Jimbo hilo kaika miradi mbali mbali ya Maendeleo.
Balozi Amina alisema miongoni mwa maeneo yaliyoguswa katika mkataba huo ni pamoja na ushirikiano ya pamoja katika mbinu za utunzaji wa mazingira kwenye Mji wa Rosha Jimboni Shadong na ule wa Zanzibar.
Ushirikiano huo pia umegusa eneo la bidhaa zinazotokana na mazao ya baharini, lakini kilichopo kwa sasa ni maendeleo ya Utafiti ya kina wa Mradi huo kabla ya kuaza utekelezaji wake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.