Habari za Punde

ZSSF Kukabidhiwa Jengo la Zamani la Hoteli ya Mkoani na Kulifanyia Ukarabati Mkubwa Kwa Ajili ya Matumizi ya Hoteli Kisiwani Pemba.

Muonekano wa Jengo la Hotel ya Mkoani baada ya kukamilika kwa Ukarabati wake Mkubwa kama linavyoonekana picha baada ya kukabidhiwa na kumkabidhi mjengo wa Ukarabati huo.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Jamii Zanzibar ZSSF.Bi. Sabra Issa Machano akimkabidhi Hati ya Makubaliano ya Ujenzi wa Ofisi za ZSSF Kisiwani Pemba Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Quality Building LTD,Ndg. Khamis Ali Shaibu, baada yac kukamilika kwa utilianaji wa Saini, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za ZSSF Tibirinzi Pemba.
Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Bi. Sabra Issa Machano akimkabidhi mchoro wa Jengo la Hoteli ya Mkoani Kisiwani Pemba Mjenzi wa Ukarabati wa Jengo Hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Engineering Co Ltd Mahir Said Ali, wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa sainiu ya ukarabati wa jengo hilo litakalokuwa na ghorofa tatu. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za ZSSF Tibirinzi Chakechake Pemba.
Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibaer ZSSF Bi. Sabra Issa Machano akitiliana saini ya Ukarabati Mkubwa wa Jengo la Hoteli ya Mkoani Kisiwani Pemba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Engineering Co Ltd  Ndg. Mahir Said Ali, ya ujenzi wa jengo hilo na kuweka samani zote katika Hoteli hiyo baada ya kukamilika ujenzi wake 
Mkurugenzi Mwendeshaii wa ZSSF Zanzibar Bi.Sabra Issa Machano, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini na makampuni yatakayokarabati Hoteli ya Mkoani na Ofisi za ZSSF Kisiwani Pemba. 
Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe.Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini ya ukarabati wa Hoteli ya Mkoani na Ofisi za ZSSF Kisiwani Pemba, iliofanyika katika ukumbi wa ZSSF Tibirizi Pemba. na kuwataka wajenzi wakamilisha ujenzi huo kwa wakati, kulia Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF.Bi. Sabra Issa Machano na kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF.Dk Suleiman Rashid Mohamed.
Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF Dk Suleiman Rashid Mohamed, aliwataka wajenzi wa majengo hayom kuhakikisha wanatekeleza agizo lililomo kwenye mikataba ya kujenga majengo yenye ubora.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.