Kiongozi wa Mahujaji wa Taasisi ya Istiqama Zanzibar Sheikh Suwedi Ali Suwedi akiwaasa mahujaji waliorudi hijja hivi karibuni kutekeleza nguzo ya tano ya kiislamu, akizungumza na Mahujaji hao katika ukumbi Baitul Yamin Malindi Mjini Zanzibar
Mahujaji waliorudi Makka kutekeleza ibada ya hijja wakimsikiliza Shekh Suweid Ali (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi wa Baitul Yamin Mjini Zanzibar.
Picha na Mwashungi Tahir wa Habari Maelezo.
Na.Mwashungi Tahir Maelezo 28-9-2019.
Mahujaji waliorejea nchini kutoka Macca Saudia Arabia kutekeleza Ibada ya Hija wamehimizwa kulinda hija zao kwa kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu ili kuweza kupata mafanikio duniani na akhera.
Wasia huo ameutoa Kiongozi wa Mahujaji kutoka Taasisi ya Istiqama Zanzibar Sheikh Suwedi Ali Suwedi huko katika ukumbi wa Bayt al Yamin Malindi mjini Zanzibar alipokuwa akizungumza na Mahujaji hao .
Alisema kuwa Mahujaji waliorejea kutekeleza Ibada hiyo wajitahidi kulinda hija zao ili ibada zao ziweze kuleta tija kwao na kuwa kigezo kizuri kwa jamii iliyowazunguka
“Wajibu kwa Mahujaji kubadilika kutokana na Ikram kubwa waliyopewa na Allah S.W kupata uwezo wa kutekeleza ibada hiyo.”alisema Sheikh Suedi.
Aidha alisema kwenda hija sio kuhiji tu na kurudi ikawa basi, bali Hija ni kukamilisha kwa moyo mmoja na kuonyesha mabadiliko ya kuwa karibu zaidi na Mwenyenzi Mungu na kuyaacha yale yote aliyoyakataza .
Alifahamisha kuwa baada ya kurudi hija kwa kumuomba Mwenyezi Mungu kakupa lakini kile alichokupa utakitunza vipi , haina maana tusile vizuri tusende katika shughuli zetu za maisha lakini lazima tuoneshe namna ya kubadilika.
“ Hija ni hii ya mwanzo hata ikikariri mara kumi mara ishirini ukenda hija basi daraja ya hija ya mwanzo ndio Mwenyezi Mungu anampa mja wake milango ya kheri na fadhila katika umri wake``. alisema Sheikh Suedi.
Aidha amewasisitiza waislamu wenye uwezo kufanya haraka katika kutekeleza ibada hiyo muhimu ili kuweza kuondoa deni baina yao na Allah S.W.
Nae Mwenyekiti wa kamati ya hija Istiqama Sheikh Sultan Khamis Mazrui amesema tathmini hiyo ina faida kubwa katika kuondosha kasoro kwa jumuiya na viongozi mmoja mmoja katika kuwasimamia mahujaji kutekeleza ibada yao kwa ubora.
Nao Mahujaji hao waliosafiri na Taasisi ya Istiqama Zanzibar wamewashukuru wasimamiaji kwa utekelezaji wa kazi zao za kusimamia Mahujaji hao katika harakati za ibada hiyo hadi kukamilika na kurejea salama.
Hata hivyo waliiomba Taasisi hiyo kuweza kujipanga vyema katika safu ya Uongozi na Usimamizi wa Mahujaji katika mwaka ujao kwani wanapofika Mji wa Makka na Madina mahujaji huwa wageni katika kila maeneo na kuweza kuepukana na usumbufu utakaoweza kujitokeza .
Pia wamewaomba waislamu wenzao wa kila mwenye uwezo afanye haraka ya kwenda Makka kufanya ibada hiyo,ikiwa wangali wazima wa Afya na wasisubirie hadi wafikie watu wazima kwani jambo lolote la ibada ukilifanya na nguvu zako ndio linakuwa bora zaidi.
“walisema raha zaidi unapokwenda kule uwe na nguvu zako kwa kuweza kufanya vitendo mwenyewe kila sehemu hapo inakuwa uzuri hasa,”walisema mahujaji hao.
No comments:
Post a Comment