Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Afungua Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Mkoa wa Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Kagera

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mvinyo uliyotengenezwa kwa kutumia ndizi, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kagera Women Group, Bertha Kokulengya, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika madini ya kopa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Tanzania Plus Minerals Kyerwa, Salim Mhando, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wajasiriamali wa kikundi cha Wanawake cha Bezaleli, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa maeneo ya uwekezaji Mkoa wa Kagera na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Benard Limbe, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wajasiriamali wa kikundi cha Wanawake cha Bezaleli, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kitabu cha muongozo wa uwekezaji katika Mkoa wa Kagera, baada ya kufungua Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Mkoa wa Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo. Agosti 14.2019. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.