Naibu Waziri wa
Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akijibu maswali leo Bungeni
Jijini Dodoma.
Na. Shamimu Nyaki
–WHUSM
Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Serikali
inaendelea kusajili Vyama na Vilabu vya michezo ikiwemo vya soka la wanawake
ili kuimarisha maendeleo ya mchezo huo chini.
Mhe.Shonza ameyasema
hayo leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe.Devotha Minja
(Viti Maalum) aliyeuliza Je ni upi mkakati wa Serikali wa kuhamasisha soka kwa
wanawake katika ngazi za Mikoa na Wilaya kuwa na timu za soka kwa wanawake kama
ilivyo kwa wanaume ?
“Serikali imekuwa
ikiandaa program mbalimbali za kukuza na kuendeleza soka la wanawake ikiwemo
michezo ya UMITASHUNTA na UMISETA na kuanzishwa kwa shule za michezo ambazo
zinadahili wanamichezo wa kike ambao moja kati ya michezo inayofundishwa ni
mpira wa miguu”amesema Mhe.Shonza.
Akijibu maswali ya
nyongeza ya Wabunge Mhe.Shonza ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha
wafadhili na wadhamini mbalimbali kufadhili na kudhamini soka la wanawake
nchini.
Aidha Mhe.Shonza
amesema kuwa mafunzo mbalimbali ya ukocha na uamuzi wa mpira wa miguu kwa
wanawake yameendelea kutolewa,sasa tunawaamuzi wanaotambulika na Shirikisho la
Mpira wa Miguu duniani (FIFA)
Halikadhalika Mhe.Shonza
amesema kuwa Serikali inaendelea kuwahamasisha wanawake kujihusisha katika
kucheza mpira wa miguu kwa kuwa ni mchezo maarufu na kwamba unatoa fursa ya
ajira kwa mtoto wa kike.
No comments:
Post a Comment