Habari za Punde

Timu ya taifa ya vijana itakayoshiriki CECAFA nchini Uganda yatajwa
Na. Hawa Ally, Zanzibar.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa 20 Nassor Salum ametangaza kikosi cha wachezaji 27 kwaajili ya kuunda timu ya Taifa ya Vijana itakayoshiriki michuano ya CECAFA nchini Uganda Sept 21 mwaka huu. 

Akitaja kikosi hicho mbele ya Waandishi wa habari Kocha Nassor amewataja mlinda mlango ni Artif Ali ( Machomane FC) , Doto Peter(Jang'ombe boys) , Ahmed Maradhi(KVZ Fc) kuwa magoli kipa 

Kwa Upande wa beki za Pembeni amewateua Nassor Khamis(Mapembeani FC) , Abdallah Said(MlandegeFc) , Haruna Rashid (Mapembeani Fc) na Nassor Juma (Malindi Fc) .
Kwa Upande wa Walinzi wa kati  ni  Saleh Mussa(ZFDC FC) , Yakoub Amour(Jang'ombe boys) , Mudathir Nassor(Chuoni FC, na Ridhiwani Mussa(Azam B) .

Aidha kiungo Mkabaji ni Mustafa Muhsini( Zimamoto FC) , Abdulaziz Rashid(ZFDC FC) na Khamad Shaaban(Rich boys) . 

Kwa upande wa Viuongo ni Sleiman Idrisa(Mapembeani FC) , Yusuph Nassor(ZFDC FC) , Mwinyi Khamis(Mkokotoni) , Ali Saleh(ZFDC FC) , Salum Hamadi (Machomane) na Mil-ghan Nahoda(Mapembeani) .

Hata hivyo Kwa upande wa washambuliaji aliwataja ni Yusuph Suleiman(Black Sailor), Mohd Ali(Biashara FC) , Fahmi Rajab (ZFDC FC) , Sadam Makame(Baraza FC) , na Dominic Kuhanga(Green lowers FC) . 

Aidha alisema Kocha Nassor amesema mchujo huo ni wa hatua ya mwanzo baada ya kucheza mechi mbili za kirafiki katika kutafuta wachezaji 20 watakaosafir nao kuelekea nchini Uganda. 

Hata hivyo timu hiyo ipo kambini  hapa  kisiwani Unguja kwaajili ya maandalizi ya mwisho ya  kuelekea michuano hiyo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.