Habari za Punde

Uzinduzi wa Mpango wa Kutokomeza Maradhi ya Kipindupindu Zanzibar.Kauli Mbiu ya Kutokomeza Kipindupindu Zanzibar “ Zanzibar Bila ya Kipindupindi Inawezekana ”

Na.Maelezo Zanzibar.                                                                                                                              
Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa  kushirikiana na Wizara ya Afya itazindua Mpango wa Kutokomeza Maradhi ya Kipindupindu Zanzibar Septemba 10,2019 .
Uzinduzi wa Mpango huo utafanyika  katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein atakuwa mgeni rasmi .
Kama inavyofahamika  Zanzibar  kuna matukio 19 ya ugonjwa wa kipindupindu tangu mwaka 1978 katika  matukio hayo watu 14364 waliugua kipindupindu na kati ya hao wagonjwa 210 walipoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu .
Takwimu hizi zinaweza kuwa ndogo kutokana na kutokuwa na takwimu sahihi kwa baadhi ya wagonjwa wa  maradhi hayo kutoripotiwa  .
Mnamo mwaka  2015 jamii yetu ya Zanzibar ilikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu ambao ulidumu kwa miezi 10 kuanzia Septemba 2015 hadi Julai  Mwaka 2016 jumla ya kesi 4330 ziliripotiwa kuathirika  na wagonjwa huo na wagonjwa 68 walipoteza maisha  .
Ugonjwa wa Kipindupindu umeripotiwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1835 ukitajwa kutoka kaskazini mwa Afrika.  Ugonjwa mkubwa wa kipindupindu  ulitokea tena Visiwani Zanzibar mwaka 1869 mpaka mwaka 1870 na watu kadhaa walifariki.

Katika muendelezo wa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu, ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuimarisha huduma za jamii  ikiwemo Afya bora, maji safi na salama, usafi wa mazingira  pamojana kutoa elimu ya afya,  kwa lengo la kutokomeza kabisa kipindupindu ifikapo mwaka 2027 kwa kuzingatia mpango wa shirika la Afya la umoja wa mataifa (WHO) wa kumaliza kabisa kipindupindu ifikapo mwaka 2030 .
Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali itaongoza Mpango wa Kutokomeza Kipindupindu Zanzibar 
Uzinduzi wa Mpango wa kutokomeza kipindupindu Zanzibar umefadhiliwa na Tassisi mbali mbali za Kimataifa zikiwemo  Shirika la Afya ulimwenguni (WHO), Mfuko wa kuhudumia watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Korea (KOIKA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.