Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe Amina Salum Ali akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo (chamber of commerce) huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara ya Biashara na Viwanda, Migombani
Washiriki wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo (chambe of Commerce) wakimsikiliza Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe Amina Salum Ali huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara ya Biashara na Viwanda,, Migombani
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo (Chamber of Commerce) Toufiq S.Turky akielezea changamoto na fursa zilizopo za kibiashara katika soko la Afrika Mashariki huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Wizara ya Biashara na Viwanda, Migombani
Na.Khadija Khamis -Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe Amina Salum Ali ameitaka Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo (chamber of commerce) kuitumia fursa walioipata ili kuingia katika ushindani wa kibiashara Kanda ya Afrika Mashariki .
Hayo aliyasema huko katika ukumbi wa Wizara ya Biashara na Viwanda, Migombani wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo katika kujipanga namna ya kuikabili fursa hiyo .
Alisema Serikali iko tayari kushirikiana na wafanyabiashara kuimarisha mikakati ya kibiashara kwa wafanyabiashara wa Zanzibar , wakubwa wakati na hata wadogo wadogo ili kuweza kuwainua kibiashara .
Alisema Wizara ya biashara na viwanda itachukua juhudi za kushirikiana katika mipango ya kuzalisha bidhaa zilizobora na zenye kiwango jambo ambalo litatasaidia kuwaongeza nguvu ya kuyatumia masoko ya afrika mashariki
Aidha aliitaka jumuiya hiyo kuyatumia masoko ya afrika mashariki ikiwemo kongo sudan msumbiji kenya ili kukuza kiwango cha kibiashara hadi ikifika julai mwakani iwe tayari matunda yameshaonekana
Hata hivyo alimpongeza Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda vidogo vidogo (chamber of commerce) Toufiq S.Turky kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Afrika Mashariki
Nae Rais wa Jumuiya ya (chamber of commerce) Toufiq S.Turky alisema gharama zinazotozwa zaidi ya mara tatu kwa mizigo zinachangia kurudisha nyuma maendeleo ya kibiashara .
Alifahamisha kuwa iwapo matatizo ya usafirishaji wa bidhaa utapofanyiwa marekebisho kwa utasaidia kukuza kiwango cha kibiashara ambacho kitafikia ushindani wa kibiashara katika afrrika ya mashariki
No comments:
Post a Comment