Habari za Punde

Rais John Magufuli aongoza sherehe za kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu  Ndugu Mzee Mkongea Ally kwenye sherehe  za Kilele za Mbio za
Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20  ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameiagiza Taasisi ya Kuzuia Rushwa Tanzania {TAKUKURU} kufanya uchambuzi na kupitia kwa kina Ripoti ya Mwenge wa Uhuru ili kubaini ufisadi uliofanywa na baadhi ya Watendaji waliopewa dhama ya kusimamia Miradi 82 iliyotiliwa mashaka katika vuguvugu la Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu.
Alisema yule atakayebainika kuhusika na ufisadi  wa kuzototesha Mradi aliyokabidhiwa  kuusimamia Taasisi ya Kuzuia na kudhibiti Rushwa Tanzania ichukuwe hatua ya kumfungulia mashataka, enmdapo ifisadi huounamuhusu Kiongozi wa ngazi ya juu apewe Taarifa yeye mwenyewe ili amuwajibishe mara moja.
Dr. John Pombne Magufuli alitoa Agizo hilo wakati wa Kilele cha Sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika Uwanja wa Ilului Mkoani Lindi, sherehe zilizoambatana na Wiki ya Vijana pamoja na Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutimia Miaka 20 tokea kifo chake.
Alisema haiwezekani Watu wachache kwa maslahi yao binafsi waendelee kuchota fedha za Walipa Kodi yaaani Wananchi zinazoingizwa na Serikali kwa ajili ya kuunga mkono Miradi ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Taifa kwa Ujumla.
Dr. Magufuli alisema Mwenge wa Uhuru utaendelea kuwa na heshima ya Taifa kwa kubainisha mapungufu yanayojichomoza katika harakati za utembezwaji wake inayokwenda sambamba na kumuenzi Baba wa Taifa kwa Kazi kubwa ya kujijengea msingi imara Taifa la Tanzania.
“ Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ataendelea kuenziwa  bila ya woga wowote kwa kuyasimamia yale yote aliyoayaanzisha wakati wa uhai wake”. Alisisitiza Dr. John Pombe Magufuli.
Alibainisha kwamba mtazamo wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wote wa Tanzania kupitia Azimio la Arusha unazidi kutekelezwa  na Awamu zote zilizopita hasa kwenye uimaeishaji wa Miundombinu ya Mawasiliano ya Bara bara na Anga.
Dr. Magufuli alieleza kwamba huduma za Afya, Elimu, Maji, zinaendelea kuimaerishwa  ili kuwaondoshea usumbufu Wananchi zinazokwenda sambamba na kasi ya Ujenzi wa Viwanda vipya vipatavyo 4,000 hivi sasa iliyolenga kuleta Ukombozi wa Kiuchumi kwa kutoa fursa zaidi ya Ajira.
Hata hivyo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alifahamisha kwamba Serikali Kuu imejikita zaidi kunawirisha Mikoa ya Kusini mwa Tanzania kwa kuchelewa kwake kupayta Maendeleo ya haraka kutokana na kujikita zaidi katika harakati za Ukombozi wa Mataifa ya Bara la Afrika.
Dr. Magufuli katika nasaha zake aliwashukuru na kuwapongeza Vijana Sita waliotembeza Mwenge wa Uhuru Mwaka Huu wakiongozwa na Mzee Mkongea Ali Kutoka Mkoa Mjini Magharibi kwa kazikubwa waliyoifanya ya kukamilisha jukumu waliokabidhiwa na Taifa.
Alisema Uzalendo wao umeitia moyo Serikali Kuu jambo ambalo Vijana wanapaswa kuwa tayari kupokea dhamana mbali mbali za Uongozi katika kulitumikia Taifa wakijitayarisha kwa kutanguliza Uzalendo mbele.
Akitoa Taarifa ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Ulemavu Mh. Jenista Joaquim Mhagama alisema Mwenge wa Uhuru umetembezwa Kilomita 26,273.94 katika Mikoa 31, ndani ya Halmashauri 195, Siku 195 na Miezi 7.
Mh. Mhagama alisema Miradi ipatayo 1,390 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Trilioni 4.7 zilizotolewa na Serikali, Taasisi na Wadau wa Maendeleo na Watu Binafsi ilizinduliwa na mengine kuwekewa Mawe ya Msingi.
Alisema mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimeweza kugundua kasoro katika Miradi 107 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 90.2 ambayo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru alikataa kuizindua na mengine kuiwekea Mawe ya Msingi kutokana na kubaini mapungufu ya cheche ya uchakachuaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Ajira na Ulemavu aliwaomba Watanzania kujiepusha mbali na kejeli zinazotyolewa na baadhi ya Watu wakidai kwamba Mkiradi inayoambatana na harakati za mbio za Mwenge wa Uhuru ni kiini macho.
Akitoa Salamu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Aman Karume alisema Falsafa ya Mwenge wa Uhuru imelenga kuwaunganisha Wananchi wote Tanzania Bara na Zanzibar katika kujenga Umoja, Uzalendo, Mshikamano na kudumisha Amani.
Alisema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameliacha Taifa la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mamani na Wananchi wake wakiendelea kushirikiana katika harakati zao za kujiletea Maendeleo bila ya kujali Itikadi zao za Kisiasa, Kidini na Kikabila.
Balozi Karume  amewapongeza Wananchi wa Mkoa wa Lindi kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya ambayo yameendana na hadhi ya sherehe  hiyo ya kuhitimisha Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu wa 2019.
Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu unasema:- Maji ni Haki ya kila Mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.