Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella amewataka Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Mwanza,
kuhakikisha wanatimiza vyema wajibu wao ili zoezi la uandikishaji wananchi kwenye
daftari la wakazi wenye sifa za kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa lifanyike kwa amani.
Mongella
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ameyasema hayo Oktoba 07, 2019 kwenye
kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Mwanza na kubainisha kwamba zoezi hilo
linatarajiwa kuanza Oktoba 08, 2019 (mwisho Oktoba 14, 2019) huku Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa ukitarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019.
Tazama Video hapa chini
No comments:
Post a Comment