Habari za Punde

SEMINA ELEKEZI YA MAKAMISHNA WA TUME YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA

Mwenyekiti wa Tume ya  Maadili Zanzibar Asaa Ahmed  Rashid akifungua mafunzo elekezi ya Makamishna ya Tume ya Haki za Binaadamu huko katika hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni .

Na Mwashungi  Tahir - Maelezo .
Mwenyekiti  wa Tume ya Maadili Zanzibar Asaa Ahmed Rashid  amewataka Makamishna wa Tume ya haki za binaadamu kuimarisha haki za binaadamu na misingi ya utawala bora kwa kuandaa mpango maalumu wa  kuwaelimisha wananchi ili  kuweza kujuwa wajibu wa kulinda na kutetea haki zao .
Akifungua Mafunzo Elekezi kwa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali  Suleiman huko katika           Ukumbi wa Hoteli Madinat Al Bahar iliopo Mbweni.  
Alisema Makamishna hao wameaminiwa na Serikali kwa  kusimamiana kuimarisha haki za binaadamu na kutoa maamuzi pamoja na kupokea malalamiko yanayowasilishwa na wananchi kwenye Tume  kwa kuzingatia Katiba na Sheria za Nchi.
Alisema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuziingiza haki za binaadamu katika katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano  ya mwaka 1977 kupita mabadiliko ya tano ya mwaka 1984.
Aidha alisema mwananchi yeyote wa Tanzania ambaye atahisi haki zake za msingi zinakiukwa anayo fursa ya kupeleka malalamiko yake mbele ya Mahakama au vyombo vyengine vilivyoanzishwa kisheria vitavyomsikiliza na kurekebisha kasoro ya ukiukwaji wa haki zitojitokeza.
Hivyo amesema mafunzo haya kwa Makamishna wa Tume  hiyo yatasaidia kujenga uwelewa na kuvielimisha vyombo mbali mbali vya Serikali na wananchi kwa jumla katika kuimarisha haki za binaadamu na misingi ya utawala bora.
" Suala la haki za binaadamu ni jambo la msingi katika nchi  zinazothamini utu , demokrasia na maendeleo ya  jamii  Makamishna wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala bora walopata dhamana kusimamia haki ",alisema Mwenyekiti huyo .
Nae Kaimu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Fatma Muya  amesema majukumu ya Tume kuzilinda kutetea haki za binaadamu katika Misingi ya Utawala Bora.
Amesema majukumu mengine ni kusikiliza malalamiko ya wananchi . matumizi mabaya ya madaraka , kuyafanyia tafiti za masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa haki za binaadamu.
Kwa upande wake Kamishna wa haki za binaadamu Zanzibar Khatibu Mwinyichande amesema kazi  zao ni  kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuwapatia haki zao zinastahiki kwa mujibu wa sheria .
Hivyo amesema Serikali imeandaa vyombo katika Tume za Haki za binaadamu kwa lengo la kusikilizwa wananchi ambao wanamalalamiko yao na kufanyiwa kazi.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu ambae ni Jaji Mstaafu Marthew Pauwa Mhina akimkaribisha Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Tume ya  Maadili Zanzibar Asaa Ahmed  Rashid katika semina elekezi ya Makamishna wa Tume ya Haki za Binaadamu huko katika Ukumbi wa Hoteli ya  Madinat Al Bahar Mbweni.

Watendaji wa Tume ya haki za binaadamu wakiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya haki za binaadamu huko katika hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni .
Picha na Khadija Khamis  Idara ya Habari Maelezo Zanzibar 

Na Mwashungi  Tahir - Maelezo       .28/11/2019
Mwenyekiti  wa Tume ya Maadili Zanzibar Asaa Ahmed Rashid  amewataka Makamishna wa Tume ya haki za binaadamu kuimarisha haki za binaadamu na misingi ya utawala bora kwa kuandaa mpango maalumu wa  kuwaelimisha wananchi ili  kuweza kujuwa wajibu wa kulinda na kutetea haki zao .
Akifungua Mafunzo Elekezi kwa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali  Suleiman huko katika           Ukumbi wa Hoteli Madinat Al Bahar iliopo Mbweni.  
Alisema Makamishna hao wameaminiwa na Serikali kwa  kusimamiana kuimarisha haki za binaadamu na kutoa maamuzi pamoja na kupokea malalamiko yanayowasilishwa na wananchi kwenye Tume  kwa kuzingatia Katiba na Sheria za Nchi.
Alisema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuziingiza haki za binaadamu katika katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano  ya mwaka 1977 kupita mabadiliko ya tano ya mwaka 1984.
Aidha alisema mwananchi yeyote wa Tanzania ambaye atahisi haki zake za msingi zinakiukwa anayo fursa ya kupeleka malalamiko yake mbele ya Mahakama au vyombo vyengine vilivyoanzishwa kisheria vitavyomsikiliza na kurekebisha kasoro ya ukiukwaji wa haki zitojitokeza.
Hivyo amesema mafunzo haya kwa Makamishna wa Tume  hiyo yatasaidia kujenga uwelewa na kuvielimisha vyombo mbali mbali vya Serikali na wananchi kwa jumla katika kuimarisha haki za binaadamu na misingi ya utawala bora.
" Suala la haki za binaadamu ni jambo la msingi katika nchi  zinazothamini utu , demokrasia na maendeleo ya  jamii  Makamishna wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala bora walopata dhamana kusimamia haki ",alisema Mwenyekiti huyo .
Nae Kaimu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Fatma Muya  amesema majukumu ya Tume kuzilinda kutetea haki za binaadamu katika Misingi ya Utawala Bora.
Amesema majukumu mengine ni kusikiliza malalamiko ya wananchi . matumizi mabaya ya madaraka , kuyafanyia tafiti za masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa haki za binaadamu.
Kwa upande wake Kamishna wa haki za binaadamu Zanzibar Khatibu Mwinyichande amesema kazi  zao ni  kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuwapatia haki zao zinastahiki kwa mujibu wa sheria .
Hivyo amesema Serikali imeandaa vyombo katika Tume za Haki za binaadamu kwa lengo la kusikilizwa wananchi ambao wanamalalamiko yao na kufanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.