Na
Anitha Jonas – WHUSM 2020Dodoma. Naibu
Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka
wazazi na familia kuwa walezi wa kwanza kwenye jukumu la kumlea mtoto.
Mheshimiwa
Shonza ametoa kauli hiyo leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali
la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Mgeni Jadi
Kadika (CUF) lilikokuwa likisema serikali haioni sasa ni wakati muafaka kwa
vijana wetu kuwekewa umri maalumu wa kutumia mitandao ili kupunguza mmomonyoko wa maadili.
Akijibu
swali hilo la msingi Mhe.Shonza alisema kuwa ni kweli utandawazi umechangia
sana katika kuleta mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa kwa jamii zetu
hususani vijana kupitia
intaneti,mitandao ya kijamii na maudhui ya nje kupitia muziki na filamu na
ndiyo maana serikali ilileta Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrime Act) ya
Mwaka 2015 pamoja na Kanuni za Maudhui ya Mtandao na Maudhui ya Redio na Runinga za Mwaka 2018.
‘’Serikali
iliiona changamoto hii mmomonyoko wa maadili na ndiyo maana ikaunda Sheria hiyo
ambayo ilipigiwa sana kelele ndani na nje ya nchi kuwa ibana uhuru ,‘’alisema
Shonza.
Mhe.Shonza
akiendeleza kuzungumza wakati ajibu swali la hilo alisisitiza kuwa familia na
wazazi ndiyo wenye jukumu la ujumla la kumlea mtoto na taasisi za elimu ya
awali,Msingi,Sekondari hadi Elimu ya Juu
ambao huwaelimisha kwa maneno na vitendo watoto na vijana kuhusu
utambuzi wa mambo mema na mabaya yanayofaa na yasiyofaa, na baada ya hatua hizo
ndipo wajibu mkubwa wa serikali unapojitokeza.
Akiendelea
kujibu swali la nyongeza la mbunge huyo lilihoji je, serikali haioni haja
kufanya kama nchi zilizoendelea kuzuia watoto kuingia katika mitandao na
kuangalia picha chafu katika mitandao,Naibu Waziri huyo alijibu kwa kusema kuwa
serikali imekwisha fanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuunda sheria
zinazosimamia masuala hayo, hivyo alitoa wito kwa viongozi kuwa wakwanza
kuzisimamia sheria hizo na alisisitiza kuwa suala la malezi ya watoto siyo la serikali
peke yake bali ni pamoja na wazazi.
No comments:
Post a Comment