Habari za Punde

Wananchi wa Kijiji cha Paje Wapata Huduma ya Macho na Miwani Kutoka Taasisi ya Sweden Huduma Hiyo Imetolewa Katika Kituo cha Afya Paje.

Mmoja kati ya Wananchi waliyojitokeza kupata huduma za macho Maua Sleiman Said akijaribu kusoma wakati akipatiwa huduma hiyo na Daktari kutoka Shirika la utoaji wa miwani la Sweden Julia Sandberg katika Kituo cha Afya Paje Wilaya ya Kusini.
Mkuu wa Kitengo kutoka Shirika la utoaji Miwani la Sweden Caroline Schiller akifanya zoezi la kumpima Macho Mtoto Kassim Juma katika Kituo cha Afya Paje.
Daktari kutoka Shirika la utoaji wa Miwani la Sweden Emma Elmebno akimpima Miwani Sofia Khamiss Juma katika hafla iliyofanyika Kituo cha Afya Paje.
Mratibu kutoka Shirika la utoaji Miwani la Sweden Happiness Urassa akitoa Maelezo kuhusu zoezi zima la kutoa huduma za macho huko Kituo cha Afya Paje.

Baadhi ya Wananchi waliofika kupata huduma za macho huko kituo cha Afya Paje Mkoa wa Kusini Unguja.
Picha Na Maryam Kidiko - Idara ya habari Maelezo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.