Habari za Punde

Wavamizi wa Kiwanja cha Programu ya Urithi na Ukombozi Bara la Afrika Mwabwepande watakiwa Kuondoka Haraka

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na MIchezo Dkt.Ally Possi (alievaa  kofia)  leo akikagua eneo la Kiwanja  ambapo kutajengwa Kituo cha  Kikuu cha Kimataifa cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika lenye ukubwa wa  ekari 65 lililopo katika Mtaa wa Mji Mpyaa Mwabwepande jijini Dar es Salaam,watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara ya Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo  na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi na Maadili ya Taifa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Bw.Boniface Kadili.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa pili kulia) akimsikiliza Afisa Mtendaji Mtaa wa Mji Mpya Mabwepande (wakwanza kulia)alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu wavamizi wa eneo la Kiwanja cha kujengwa Kituo Kikuu cha  Programu ya Urithi wa Ukombozi  wa Bara la Afrika  alipofanya ziara kukagua kiwanja hicho leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na MIchezo Dkt.Ally Possi (aliyevaa kofia)wa akikikagua baadhi ya barua za  mmoja wa  watu wanapoishi alizoziandika Wilaya ya Kinondoni  akidai eneo hilo kuwa ni la wazazi wake, alipofanya ziara ya kukagua kiwanja hicho leo jijini Dar es Salaam, Kiwanja  hicho kitakacho jengwa, Kituo Kikuu cha  Programu ya Urithi wa Ukombozi  wa Bara la Afrika  ambapo alikuta kuna wananchi wamevamia wanaishi katika eneo hilo mbali na kuwa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kuwa wameshapewa hati yakiwanja hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.