Habari za Punde

Wadau wa Masuala ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Wanakutana Kujadili Utekelezaji wa MTAKUWWA

Mkurugenzi Mtendaji kutoka TECDEN (Tanzania Early Childhood Development Network) Bw. Bruno Ghumpi akifafanua jambo wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpango Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kilichofanyika Februari 6, 2020 katika Ukumbi wa mikutano wa Flomi hotel Morogoro.
Mratibu wa Taifa wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Bi. Happiness Mugyabuso (katikati) pamoja na Katibu wa kikao hicho Bw. Mwendesha Makelemo na Mratibu wa Mpango huo kutoka TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga (wa kwanza kushoto) wakifuatilia hoja za kikao hicho.
Wajumbe wa kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpango wa Kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wakifuatilia hoja wakati wa kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Bi. Rennie Gondwe akiwasilisha mada wakati wa kikao hicho.
Mratibu wa Mpango wa Kutokomea Kukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kutoka TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga akifafanua hoja wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Mpango huo.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.