Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi za SADC
wakizunguka katika mbuyu wenye umri wa Zaidi ya miaka 500 uliopo katika mji wa
kihistoria KAOLE Bagamaoyo walipotembelea baada ya kumaliza Mkutano wa Mwaziri
wa Kazi na Ajira na Wadau wa utatu wa Nchi za SADC ulifanyika Machi 5, 2020
JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi za SADC wakipata
maelezo kutoka kwa mwongoza watalii wa makumbusho ya mji wa bagamoyo kuhusu
kaburi la Binti Sharrfa sharifu aliyekuwa na nguvu za Ajabu na alifarika akiwa
na umri wa miaka 13 katika mji wa
kihistoria KAOLE walipotembelea baada ya kumaliza Mkutano wa Mwaziri wa
Kazi na Ajira na Wadau wa utatu wa Nchi za SADC ulifanyika Machi 5, 2020 JNICC
Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Ajira, Kazi, Uzalishaji na Maendeleo ya
Ujuzi wa Botswana, Mhe.Mpho Balopi akipiga ngoma za kikundi cha Utamaduni
kutoka chuo cha Sanaa Bagamoyo TASUBA, kabla ya kutembelea makumbusho ya
kihistoria KAOLE Bagamoyo, wanashuhudia kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu, Mhe.Jenista
Mhagama na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainabu Kawawa.
Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi za SADC wakinawa
maji ya kisima cha Baraka kisichokauka wala kuongezeka maji yake yaliyo mita
mbili kilichoko katika makumbusho ya KAOLE Bagamoyo walipotembelea baada ya
kumaliza Mkutano wa Mwaziri wa Kazi na Ajira na Wadau wa utatu wa Nchi za SADC
ulifanyika Machi 5, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu,
Mhe.Jenista Mhagama, akizungumza kwa Mawaziri wa Kazi na Ajira mara baada ya
kuwasili kutalii katika makumbusho ya Kaole yaliyoko mji wa Bagamoyo Pwani, ili
kujionea historia mbalimbali za wenyeji wa mji huo, Mawaziri hao walitembelea
baada ya kumaliza Mkutano wao ulifanyika Machi 5, 2020 JNICC Jijini Dar es
Salaam, Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu, Mhe.Jenista Mhagama akiwa na wageni
wake(Mawaziri wa Kazi na Ajira Nchi za SADC) baada ya kutembelea Ngome kongwe katika makumbusho ya kihistoria yaliyoko Mji wa Bagamoyo walipotembelea baada
ya kumaliza Mkutano wa Mwaziri wa Kazi na Ajira na Wadau wa utatu wa Nchi za
SADC ulifanyika Machi 5, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka SADC waliosimama
mbele wakiwa pamoja na wanafunzi wa mafunzo ya Ufundi katika fani mbalimbali
walioko katika Chuo cha Don Bosco Jijini Dar es Salaam walipotembelea kujifunza
baada ya Mkutano wa Mwaziri wa Kazi na Ajira na Wadau wa utatu wa Nchi za SADC
ulifanyika Machi 5, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu, Mhe.Jenista Mhagama akitoa maelezo kwa
wageni wake(Mawaziri wa Kazi na Ajira Nchi za SADC) mara baada ya kuwasili
Ngome kongwe katika makumbusho ya kihistoria Mji wa Bagamoyo walipotembelea
baada ya kumaliza Mkutano wa Mwaziri wa Kazi na Ajira na Wadau wa utatu wa Nchi
za SADC ulifanyika Machi 5, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wanafunzi
wa Fani ya Ufundi magari kutoka chuo cha Don Bosco Jijini Dar es Salaam,
wakionesha jinsi ya kurekebisha magari mbele ya Mawaziri wa Kazi na Ajira wa
Nchi za Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC (hawapo pichani) walipotembelea katika
Chuo hicho kujifunza jinsi programu ya mafunzo ya ufundi katika Fani mbalimbali
inavyofanyakazi ambapo Serikali ya Tanzania inawafadhili wanafunzi hao kupata
mafunzo hayo
No comments:
Post a Comment