Habari za Punde

Maandalizi ya Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru Mkoa wac Kusini Unguja.

 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Kusini Unguja Huko  Ukumbi wa Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.

Baadhi ya Waandishi wa habari Wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud akielezea kuhusu maandalizi ya Uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Kusini Ungaja hafla iliyofanyika Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
Picha Na Maryam  Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Na.Bahati Habibu   Maelezo Zanzibar  12/3/2020
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka wananchi wa mkoa huo kuhudhuria kwa wingi siku ya uzinduzi wa mbio za Mwenge zitakazofanyika huko Makunduchi
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale, Kikwajuni Mkuu wa Mkoa huyo amesema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 2 Aprili mwaka huu katika kiwanja cha Mwehe Makunduchi.
Ameeleza kuwa taratibu za maandalizi zinaendelea na tayari zimefikia katika hatua ya kuridhisha kukamilisha maandalizi hayo.
“Maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge umekamilika kwa kutayarisha kiwanja  ambacho kitafanyika uzinduzi huo pamoja na kufikisha huduma ya maji, umeme na vyoo ambapo huduma hizo zinatarajiwa kukamika ndani ya mwezi huu”, ameeleza.
 Aidha Mkuu wa Mkoa amefahamisha kuwa lengo la kutembeza mwenge  nchini ni kushiriki kwa pamoja katika kuleta Maendeleo bila ya kubagua itikadi ya  chama cha siasa  , rangi, kabila au dini  hivyo kila mwananchi ni wajibu kushiriki katika uzinduzi huo.
Hata hivyo amewataka wananchi kushirikiana kushiriki katika uzinduzi wa huo ili kuweza kufanikisha kwa lengo la kuleta maendeleo nchini
Mwenge huo wa uhuru utakimbizwa katika mkoa wa Kusini kwa muda wa siku mbili na baadae kukabidhiwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kuendelea na mbio zake
Mwenge huo wa uhuru mwaka huu umebeba kauli mbiu, “Uzalendo ni msingi wa Maendeleo ya nchi tujitokeze kupiga kura kwa amani”.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.