Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ashuhudia Utiaji wa Saini Kwa Viongozi wa Taasisi za Dini Tanzania.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe.Job Ndugai  (wa pili kushoto ) wakishuhudia wakati viongozi wa dini walipotia saini Tamko Rasmi la Viongozi wa Juu wa Taasisi za  Dini kuhusu ushiriki wao katika mwitikio wa UMKIMWI nchini, wakati Waziri Mkuu alipozindua kampeni ya kitaifa  ya viongozi wa dini na bunge  katika kupunguza unyanyapaa dhidi ya  UKIMWI kwenye ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma, Machi 10, 2020.
Viongozi  waliotia saini kutoka kushoto ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Zubeir Bin Ali Mbwana, Askofu Peter Konki  kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste,  Akofu Mkuu wa Jimbo la Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu  Katoliki Tanzania, Gervas Nyisonga,  Askofu Mkuu wa Jimbo la Kusini mwa Tanzania wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Mark Malekana na kulia ni  Mwenyekiti wa Jumuiya Kikristo Tanzania, Askfu Dkt. Alinikisa Cheyo.  Kushoto kwa Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa  Baraza la Watu Wanaoishi  na UKIMWI, (NACOPHA), Leticia  Kapela na kulia kwa Spika ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini na Mkuu wa Kanisa hilo, Dkt. Frederick Shoo.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.